WAPENZI WA KUNDI LA MAKOMA BADO WAMUWAZA NATHALIE ALIYEJITOA

Nathalie akiwa na mumewe bwana JC Atamboto
Ikiwa takribani miaka 10 tangu kujitoa katika kundi la Makoma bado wapenzi wa kundi hilo wameonyesha mapenzi yao ya dhati kwa nyota huyo wa zamani Nathalie Makoma ambaye alikuwa mwimbaji tegemewa katika kuanzisha nyimbo katika kundi hilo hususani katika toleo lao la kwanza.

Makoma kupitia ukurasa wao wa Facebook hivi karibuni waliamua kuwauliza mashabiki wao ni mwimbaji gani katika kundi hilo wampendaye ambapo kura nyingi zilimwangukia Nathalie hata lilipokuja suala la kuwauliza nyimbo wanazopenda za kundi hilo, album yao iliyowatambulisha ya 'No Jesus No life' bado nyimbo zake zimeendelea kupendwa na mashabiki wa kundi hilo sehemu mbalimbali duniani.

Kundi la Makoma
Nathalie ambaye kwasasa anaishi jijini London nchini Uingereza baada ya kuhama kutoka Uholanzi, alijitoa kwenye kundi hilo la wanandugu na kuamua kwenda kupiga muziki wa dunia, sambamba na kushiriki kwenye mashindano ya uimbaji huku ikidaiwa kwamba sababu iliyosababisha kujitoa kwake ni maelewano mabaya na kaka yake. Hata hivyo baada ya miaka kupita Nathalie ameanza kuwasiliana na ndugu zake tena ingawa bado anaendelea kimuiziki peke yake pamoja na mumewe na sasa wanatarajiwa kupata mtoto mwingine wa pili baada ya kwanza waliyempata aitwaye Giovani

Nathalie mwenye nywele zilizopakwa rangi alipoanza kutembeleana na ndugu zake mapema 2013
Nathalie akiwa na kaka yake Duma ambaye inadaiwa walikuwa hawaelewani naye

Jikumbushe Enzi hizo 'Napesi Nayo' kutoka kwao MAKOMA


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.