CHAGUO LA GK: AMETENDA MAAJABU/JINA LAKO LA AJABU KUTOKA KWA WAKOREA

Kwaya ya Gracias katika mojawapo ya kambi za IYF Afrika, nchini Tanzania mwaka 2015. ©Gracias Choir Flickr

Katika Chaguo la GK kwa Jumapili hii ya mwisho, tuko na kwaya ya Gracias kutoka nchini Korea Kusini, ambao wanafahamika zaidi kwa nyimbo za mataifa mbalimbali, ikiwemo nyimbo za Kiswahili kipekee katika kumsifu Mungu.

Gracias Choir imeundwa mwaka 200 na kundi la waimbaji mbalimbali kwa lengo la kutaka kumshukuru Mungu kutokana na uzima waliopewa. Na kama jina lao lisemavyo (Gracias kwa Kiispaniola) linamaanisha ahsante - wako kwa lengo hilo kuu.

Pata nyimbo mbili kutoka kwa kwaya hii ambayo mwaka 2013 ilifanikwia kuja Tanzania kwa mualiko wa Rais Kikwete. Ametenda Maajabu, pamoja na Jina lako la ajabu BWANA.

Upekee wa uimbaji wao ni namna wanavyotumia vyombo vyao kutengeneza ala zenye ustadi ulio bora, kuongezea na mpangilio wa sauti zao. Tuabudu nao kwa pamoja na nyimbo zao hizi mbili.

Ametenda Maajabu


Jina lako la AjabuKwa faida yako pia, unaweza kutazama video fupi kuhusiana na kwaya hii.


Tukutane wiki ijayo...

Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.