CHAGUO LA GK: UTUKUFU UMESHUKA - SHANGWE PHOSTINY

Tunatumai u salama mdau wa GK kwa Jumapili ya kwanza ya mwezi Septemba. Uzima tulionao ni jambo la kumshukuru Mungu kwayo.

Nasi katika Chaguo la GK tunakuletea Shangwe Phostiny, ambaye anatuongoza katika kumsifu Mungu kupitia wimbo unaobeba jina la album yake ya kwanza, Utukufu Umeshuka.

Album hii imerekodiwa mwaka 2013, na video yake kurekodiwa mwaka 2014 kipindi Shangwe anamaliza kidato cha nne.

Hakika fadhili zake kwetu sisi ni za milele,na halinganishwi wala kufananishwa na kitu chochote kamwe.

Tukutane Jumapili ijayo.
Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.