FAMILIA YA KWETU PAZURI YAZIDI KUONGEZEKA, KUFANYA TAMASHA KUBWA LA MIAKA 20 MWAKA HUUIkiwa miezi miwili imebaki kabla ya kufanyika kwa tamasha kubwa la shukrani kwa kwaya maarufu nchini Rwanda ya Ambassadors of Christ 'Kweu Pazuri' kutimiza miaka 20 ya huduma, kundi hilo hapo jana limetangaza habari njema za kupata mtoto kwa waimbaji wao nyota waliooana mapema mwaka jana Gicari na Joe Mutabazi ambao wamepata mtoto wa kike waliyempa jina la Malka Mutabazi

Kwaya ya Kwetu pazuri ambayo mara ya mwisho kukanyaga nchini ilikuwa wakati ilipoalikwa
kwenye tamasha la pasaka lililoandaliwa na Msama Promotions huku kwaya hiyo ikishiriki kwakukosa sapoti kutoka kanisa lao la hapa Tanzania la Sabato ikidaiwa kwaya hiyo kushiriki tamasha kama hilo ilikuwa kinyume cha kanisa hilo. Hata hivyo kwaya hiyo imeendelea kutamba na kupata mialiko mingi nchi nyingine kama Zambia, Uganda bila kusahau Kenya.

Ambapo tamasha lao la shukrani la kutimiza miaka 20 wamelipa jina la 'Ebenezer' linatarajiwa kufanyika nchini Rwanda mwezi December 24 mwaka huu, huku waimbaji waliowahi kushiriki na kwaya hiyo wanatarajiwa kuungana na wenzao siku hiyo pamoja na wazazi wa waimbaji waliofariki katika ajali ya gari iliyowapata waimbaji hao takribani miaka sita iliyopita walipokuwa wakitokea Tanzania wakirejea nchini Rwanda. 

Baadhi ya waimbaji wa Ambassadors wakiwa wanarekodi DVD mpya itakayozinduliwa wakati wa tamasha lao

Jikumbushe wimbo 'Upendo' kutoka kwao Ambassadors of Christ 

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.