JUMAPILI HII ITAKUWA YA KUKUMBUKWA KATIKA HISTORIA YA MUZIKI WA INJILI TANZANIA, USIKOSE

John Lisu akizungumza na wanahabari, kushoto mwimbaji Mercy Masika (Kenya), Angel Bernard na Bomby Johnson
Jumapili hii ya Octoba 2 itakuwa ni jumapili ya tofauti kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na wale walio jirani na jiji hilo. Siku hiyo muimbaji wa nyimbo za injili muabudu  (The worshiper) John Lisu atazindua album yake mpya iitwayo Mtakatifu  (Worth of our worship).

Akizungumzia uzinduzi huo muimbaji John Lisu amesema uzinduzi utafanyika katika kanisa la City Christian Centre  (CCC) ambalo lipo Upanga. Uzinduzi utaanza majira ya saa tisa Alasiri huku pia waimbaji kutoka Kenya na Tanzania ambao wataimba live watamsindikiza John Lisu. Waimbaji hao Mercy Masika  ( kutoka Kenya) ambaye anafanya vizuri na wimbo wenye maneno "NA SIWEZI JIZUIA KUSEMA WAKO WEMA, SIO KAMA NAJIGAMBA UMENITENDA VYEMA".

 Pia atakuwepo Angel Bernard, Bomby Johnson, Sam Yona, Aberdnego and the worshipers (kutokea City of praise Arusha ) pia atakuwepo Hulda Vagen kutoka Congo ambaye anao wimbo wenye maneno " NIMEPATA SALAMA AMBAYO DUNIA ISINGEWEZA KUNIPA".

Tiketi za uzinduzi huo zimeshaanza kuuzwa ikiwa VIP ni sh 20000 na Kawaida ni Sh 10000 na zinapatikana Mlimani City Silverspoon, Puma petrol station Mwenge, na Msama Shop posta mtaa wa mkwepu.

Mercy, John na Angel

John, Angel na Bomby

Mercy, John na Angel

Jikumbushe wimbo 'Upendo'kutoka Live DVD iliyopita ya Uko Hapa yake  John Lisu

Share on Google Plus

About Silas Mbise

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.