MPIGIE KURA NYOTA WA INJILI TANZANIA KATIKA TUZO ZA INJILI MAREKANI


Mwimbaji nyota nchini Upendo J'Bride zamani akijulikana kama Upendo Kilahiro amepiga hatua kimataifa baada ya kuchaguliwa kuwania tuzo nne zifahamikazo kama 'Gospel Safari Music Award' zitakazotolewa tarehe 22 October huko Minnesota nchini Marekani.

Akizungumza na GK kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno, Upendo amemshukuru Mungu kwakuteuliwa kwake kuwania tuzo hizo, na kuitaka GK kufikisha habari hii njema kwa wapendwa wote, wapenzi wa muziki wa injili na watanzania kwa ujumla kumpiga kura katika vipengele vyote vinne alivyopendekezwa ili basi tuzo hizo zije nchini Tanzania.

Vipengele alivyopendekezwa ni pamoja na African Traditional Gospel song of the year, 2. Gospel Female Vocalist of the year, 3.Gospel Album of the year na Gospel Song of the year

Ili kumumpigia kura Upendo ingia kwenye tovuti hii ya www.gsmtvnetwork.com ambamo ndimo inapatikana link ya kumpigia kura. Piga kura mara nyingi uwezavyo, pia shirikiana na wengine ili wapate kumpigia kura nyota wetu wa injili.

Wakati huo huo, kwa wale wote wapenzi wa mwimbaji huyu mkae tayari kupata album yake mpya ambayo kwahakika imeandaliwa katika viwango vya juu kuanzia, ujumbe mpaka uimbaji bila kusahau kwamba kuna nyimbo kama 'Mungu Unaishi' ambao ameuimba upya kwa vionjo vya rhumba na lugha tofauti.


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.