SOMO: KOMBOA LANGO LA MUDA WAKO ILI UPATE ULICHOPOTEZA

*NA MWL CHRISTOPHER E.A.  MWAKASEGE*

*TAREHE 7 SEPT 2016*.

*SIKU YA 4*

*KOMBOA LANGO LA MUDA WAKO ILI UPATE ULICHOPOTEZA*

Bwana Yesu asifiwe baada ya kunangalia mambo mawili, *FIKRA NA SHERIA* Leo tuendelee na kipingele kingine.

*KIPENGELE CHA TATU*. *MUDA WAKO WA KUABUDU*
*Marko 7:7-6* _’’Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami; *Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu* ’’_

>>Maandiko matakatifu yanasema watu humshemu Mungu kwa midomo yao bali mioyo yao iko mbali nae na hawapati faida yoyote kwa sababu tu ya kutomwabudu Mungu vizuri. Na hapa tunaona ya kuwa ukipata muda wako wa kumwabudu Mungu binafsi unakuwa umepata kitu kikubwa sana

*Unapomuabudu Mungu zingatia yafuatayo*

*1* Unapomuabudu Mungu inatakiwa upate faida na hutakiwa kumuabudu Mungu bure
*2* Unahitaji kuzijua faida unazotakiwa kuzipata kwa kumuabudu Mungu ili usipozipata basi ujue kuwa umemwabudu Mungu bure yaani hujafaidika na chochote. Ni sawa na mtu anaingiza fedha zake kwenye biashara na asimabulie chochote kwenye biashara yake kwa sababu ya kutojua tofauti kati ya fedha zake na faida au hajajua kupata faida.

*Warumi 12:1-2*_Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, *ndiyo ibada yenu yenye maana*. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu_

>>Mstari wa kwanza unazungumzia kushiri ibada yenye maana.  *Na kuna faida zake za kushiriki ibada yaenye maana*

*Faida ya kwanza* *Mungu kuingilia kati maisha yako ili akusaidie usije ukufuatisha kawaida ya dunia hii katika kumuabudu Mungu*
>>Ibada yenye maana ni lazima upate faida ndani yake. Mungu anakuwa anaingilia kati maisha yako na kukufanya utembee kwenye mapenzi yake.

*Faida ya Pili**Ikiwa kuabudu Mungu kuna uhusiano na kujulikana kwa mapenzi ya Mungu kwa yule aabuduye ina maana pia ya kuwa kuabudu Mungu kunawafungulia mlango wa wakati uliobeba maisha ya mtu anayeabudu Mungu *
>>Lingalisha Warumi 12:1-2 na Waefeso 5:15-17, Katika Warumi tunaona uhusiano wa Ibada na mapenzi ya Mungu au kuyajua mapenzi ya Mungu.12:2b ‘’*mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu*

>>Katika Waefeso kuna uhusiano kati ya wakati na mapenzi ya Mungu.  Angalia 5:17 ‘’ *Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana*
>>Kuabudu= na kuyajua mapenzi ya Mungu, kwa hiyo kama upo uhusiano wa kuabudu, wakati na mapenzi ya Mungu. Rejea tena hapo linganisha warumi na waefeso ndio utapata haya mambo.

*Faida ya tatu**Muda wa kuabudu unampa Mungu nafasi ya kukutana na mtu ambaye anataka kumfungulia lango la muda Fulani unaohusu maisha yake.

>>*Yohana 4:20-24* _Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia. Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, *saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu*_

_Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. *Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu*. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli_

>>Yesu anataka tujue kwenye saa ambayo Mungu anataka kuabuduiwa anataka akutane na watu wanaomuabudu katika roho na kweli na waweze faidika katika kuabudu kwao, na yeye ajibu mahitaji yao Angalia *mstari wa 23*

>>Mungu hatafuti jingo la ibada au nyimbo za kuabudu ali anamtafuta mtu aliyendani ya ibada na ndiye aabudu. Na Pia Mungu hatufi sadaka bali anatafuta mtoa sadaka maana si kila naetoa sadaka anamuabudu Mungu.

*MFANO*
*Mfano wa kwanza* *Matendo ya Mitume 13:1-3*  hapa tunaona walikuwa watu watano wanaabudu hapo katika ibada na Paulo na Barnaba walikuwepo jumla yao wote walikuwa ni watano, na kati ya watu hawa watano Roho Mtakatifu alisema nitengeeni hawa wawili yaani Paulo na Barnaba. Na ile hali ya kusema nitengeeni ina maana walikuwa wamechanganyika mahali ambapo hawakutakiwa kuwepo. Ndio maana Mungu alikuwa anaingilia kati maisha yao *ili arekebishe namna yakutembea kwao na watembee kwenye kusudi la Bwana*. Mungu alipoona kuabudu kwa hawa wawili kulikuwa hamna namna ya kunyamaza maana waliakuwa wanaabudu kweli, na kumbuka walikuwa watano lakini Mungu alipata wawili tu yaani Paulo na Barnaba.

>>Usimwabudu Mungu bure pata faida ndani yake maana ibada yako yako itakuwa na maana kwako na kwa Mungu pia

*Mfano wa Pili* *Mwanzo 22:1-5 ‘’ _Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia_
_Ibrahimu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu. Siku ya tatu Ibrahimu akainua macho yake, akapaona mahali pakali mbali. Ibrahimu akawaambia vijana wake, Kaeni ninyi hapa pamoja na punda, na mimi na kijana tutakwenda kule, tukaabudu, na kuwarudia tena_

>>Mungu hakuwa na shida na sadaka bali alikuwa anamtaka Ibrahimu. Na Ibrahimu alipokutana na Mungu alinufaika kwa kuwa kuna lango la Baraka lilifunguka ambalo lilibadilisha kabisa maisha yake. Na Mungu aliposema *sasa najua* ina maana kuna kitu Mungu alikiachilia katika maisha ya Ibrahimu na akawa lango la kupitisha Baraka japo aliahidiwa tokea anaoka uri ya wakaldayo lakini mlango wake ulifunguliwa baada ya kumuabudu Mungu na kufaidika na yeye.

*Faida ya nne**Anayemuabudu Mungu na akiweza kumuabudu katika saa ambayo Mungu anataka kuabudiwa atapata 

             *Jambo la kwanza* *Atapata jinsi ya kuabudu*
Shida sana ya watu wengi wanataka kumuabudu Mungu kwa staili yao na ndio maana biblia katika Marko imesema msifuatishe kawaida ya dunia hii na mapokeo ya wanadamu badala ya kufuata Mungu anavyotaka tumuabudu. Ikifika saa ya kumuabudu Mungu usitafute wimbo wa kumuabudu Mungu bali tafuta kumuabudu Mungu maana kuna tofauti ya kuimba wimbo wa kuabudu na kumuabudu MUNGU

>>Ninapopanda madhabahuni huwa kwanza nasikia wimbo kutoka juu, maana Mungu anabuduiwa kwa masaa 24 na kama anaabudiwa na akija na uwepo wake ina maana anakuja na wimbo kwa hiyo ni lazima kujua wakati huo Mungu anaabudiwa na wimbo gani huko mbinguni ili nasisi hapa tujiconect nao. Sasa shida inakuja pale nimesikia wimbo mimi na wenzangu hawajasikia ule wimbo unakuta hata ule uwepo wa Bwana unakatika. Kwa hiyo ni jukumu letu kuomba ili Mungu anapotaka kuabudiwa na wimbo Fulani kila mtu ajue hasa waimbaji wanaotuongoza ili tuweze kwendana kwa pamoja.

*Jambo la Pili* *Mungu anajifunua kwako binafsi na kuabudu ni uhusiano wako na Mungu katika ngazi ya upekee.
>>Ndio maana pakatifu pa pakatifu hatuingii kigroup bali unaingia wewe mwenyewe yaani peke yako na Mungu. Na ukiwa katika hali hiyo Mungu anakuwa anajifunua binafsi na kama sio hivyo basi unakuwa *unasali* na sio *kuabudu* au unakuwa unasikiliza tu mahubiri na kushangilia maana kusikiliza mahubiri sio kumuabudu Mungu.

*Faida ya tano** Atakuunganisha na lango lake la maisha ambalo amekupangia nawe ili uishi sawa sawa na mapenzi ya Mungu*
>>Hii ni saa muhimu sana kwako na kwa Mungu maana Mungu anakuwa anakupa muda wake na wewe unampa Muda wako.

*Faida ya sita** Mungu anatumia vigezo gani ili kumpata mtu anayetaka kumuabudu Mungu?*
    >Biblia inatumabia kuwa baba anawatafuta watu kama hao wamuabudu,
    >Katika biblia huwa tunaona Mungu vitu anavyotafuta
            *1* Kilichopotea
            *2* Watenda kazi
            *3* Mtu wa kujenga boma
>>Ukiangalia Yohana 4:21,23. Tunajifuza yafuatayo kuwa katika zamani zile Mungu alikuwa anangalia kwanza eneo la kuabudiwa kwa sababu hata hema lilikuwa linawekwa vizuri sana. Sasa mambo yamebadilika na Mungu anaangalia kwanza mtu ndipo eneo linafuata. Na Mungu anapomuangalia mtu anayeabudu haangali aina ya mtu anavyoabudu bali anamtaka mtu kwanza awe tayari na ndipo Mungu aweze kumfundisha huyo jinsi inavyotakiwa kumuabudu Mungu. Maana Mungu akitafuta waimbaji atawapata ila akitafuta muabudu anaweza asimpate hata mmoja.

*Mfano kwenye kongamano moja la maombi ya kitaifa tualolifanya kule Dodoma* siku moja tulikuwa na meza ya Bwana na Nguvu za Mungu zilitushukia maana tulikuwa Zaidi ya watu elfu tano tulioshiriki. Wakati wa jioni tunapumzika mchungaji mmoja akaja kuniuliza Mwakasege naomba nikuulize na nikasema uliza tu, akasema mbona mimi na watu wangu tukishiri kuwaga hatuoni hali ya namna hii nguvu za Mungu kutufunika namna hii.  Na mimi nikamuuliza swali kuwa je huwa unawafundisha watu umuhimu wa kushiriki meza ya Bwana. Akasema hapa, sasa nikamuuliza tena kuwa je Imani wanaipata wapi, maana Imani huja kwa kusikia. Na wasiposhiriki kwa Imani haiwezekani kumpoendeza Mungu maana *Pasipo Imani haiwekani kumpendeza Mungu*

>>Mungu anatafuta mtu kwanza ndipo baadae ampe mbinu za namna bora ya kumuabudu yeye. Na hujiulizi kwanini Mungu akufundishe kuwa mume kwanza wakati hauna mpango wa kuwa mume. Sijui unanielewa ninachosema, maana kuna wengine hawako tayari kuwa waume ila wanao tu ili kuongeza list kuwa na yeye kaoa.

>>Katika *Warumi 12:1-2*  Mungu huwa anaenda ndani ya mtu iki kumfanya awe na Ibada yenye maana na asimwabudu Mungu bure yaani bila kupata faida.

*Katika kumuabudu Mungu hutafuta mambo yafuatayo*

*1* _*Kumuabudu Mungu ni msimamo wa watu ndio huwa unampa Mungu kujua kuwa ndani yake huyo mtu Mungu kapewa nafasi yake kama Mungu.  Na Mungu anazuia usiwe na miungu mingine  maana kila Mungu anatafuta nafasi yake ya kipekee ndani ya mtu ya kuabudiwa. Mtu anayetumia muda wake mwingi kukaa uweponi mwa Mungu wake huwa anakuwa na msimamo wa aina Fulani ambayao hauyumbishwi kabisa*_

*2*_*Mtu anayejua kwanza Mungu ni nani kwake, yaani anatafuta uhusiano nae badala ya kutafuta matendo ya Mungu kwake. Maana kuna kuwa na tofauti ya mtu anayejenga mahusiano na Mungu wake na mwingine anayemwomba Mungu kwake. Si mar azote Mungu anapenda kila mda kusikiliza tu mahitaji wa watu wake na yeye anatafuta muda wa watu wake kukaa nao na kufarahi pamoja yaani fellowship nao*_
*3*_*Kuangalia uhitaji ulionao au kiu unayotaka kumpa Mungu nafasi ndani yako* _ Mungu anakataza kuvitumikia vitu bali anataka yeye ndio tumpe nafasi ya kumtumikia. Na kumbuka hili *kumtumikia Mungu kunakuja baada ya kumuabudu Mungu na kama ukifuata kanuni hii Mungu atatoa na wewe muda wake*
*Faida ya saba**Mungu huwa anakutumia wito wa kumuabudu kabla ya saa ya kukuutanisha na yeye kuabudu kama anavyotaka*
>> *Yohana 4:21,23* waabuduo halisi watamuabudu baba katika roho na kweli,na kuona kuna waabuduo halisi ina maana wapo na waabuduo feki. Na anaposema *saa ipo* kwanini anasema saa ipo na kwanini inakuja na kama inakuja ni kwanini ipo?

>>Saa inakuja maana yake ni muhimu sana usije ukakosa hiyo saa yaani ni saa muhimu sana kwako maana inakuja na kiu ya aina yake ya kuabudu.  *Na ukiona unakuwa na kiu ya kumuabudu Mungu ujue ni dalili ya kuwa saa hiyo imefika na nakumbia usioange kuikosa au ukaahirisha na ukaanza kufanya mambo mengine*

>>Mungu anapotafuta watenda kazi, hutuma wito kwanza sasa cha kushangaza unakuta mtu akipata wito tu anaanza kutumika. Swali ni kwamba unaitwa kwenye interview ila wewe unaanza kazi wakati hata mkataba wa kazi hauna.  Mungu anasema saa inakuja ina maana ni wito unaokuandaa kwa ajili ya kuabudu na angalia sana usije ukaabudu bure.

*Faida ya nane**Jitenge na vinavyokuzuia kumuabudu Mungu katika uzuri wa utakatifu wake.

*Zaburi 96:9*  _*Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu, Tetemekeni mbele zake, nchi yote*_
>>Mtakatifu ni Zaidi ya kutokuwa na dhambi na ina maana utakatifu ni kutengwa kwa hiyo hata kama ni dhambi inakuzuia kumuabudu Mungu uwe na uhakika ataitenga kwako ili uweze kumuabudu kikamilifu.
*Marko 7:6-9* Je unatumbia njia ipi kumuabudu Mungu je ni kwa mapokeo ya kwenu au? Ni Muhimu sana umkabidhi Mungu masikio yako ili uweze kusikia namna anavyokuambia umuabudu.

>>Ibrahimu alipompata Isaka alianza kujisahau ina maana taratibu akaanza kuhamisha Imani yake kutoka kwa Mungu na kupeleka kwa Isaka maana ndipo alijua Baraka zake zitapita hapo. Na uhusiano wake na Mungu ulianza kupungua na ile hali ya Mungu kuabudiwa ndani ya Ibrahimu ilianza kupungua. Ndipo Mungu akamwambia Ibrahimu amtoe Isaka ili Isaka kwake awe kama amekufa na abaki akimwangalia Mungu peke yake. Maana Mungu alijua Ibrahimu akiendelea vile asingeweza kumfaidi Mungu wake vizuri.

>>MUNGU anapokuletea kiu ndani yako ya kutaka kumuabudu yeye anataka Fikra zako zimwelekee yeye na nafsi yako pia imuelekee yeye. Huwa nikisoma habari za Adamu huwa nasikitika sana, maana Mungu alikuja kujidhihirisha kwa Ibrahimu katika hali ya mwili lakini Adamu alikuwa kapoteza nafsi yake kwa Mungu. Na Mungu alijua pia kuwa kapoteza nafsi ndani Adamu. Ukipoteza nafasi kwa Mungu wako na anajua kapoteza nafsi yake kwako oooh hii ni huzuni sana.
>>Roho ya kumuabudu Mungu inakudai nafasi ya kumuweka Mungu kwanza, kama ni mwili wako unakusumbua basi ukabidhi kwa Bwana, kama ni watoto au kazi au mume au huduma au utumishi uweke kwa Mungu kwanza ili Mungu apate nafasi ya kwanza kwako.

>>Ukisoma kitabu cha Hesabu 17 Mungu alimwambia Musa kuwa ikiwa wana wa Israel wanajua kuna mtu aliyebora kuliko Haruni waweke fimbo zao hapo madhabahuni pamoja na fimbo ya Haruni. Na Fimbo ya haruni ilichanua na zile zingine hazikuchanua. Kuwapendezesha wanadamu kusikutenganishe na Mungu wako. Katika maisha yako tutajua kuwa unahusiano na Bwana au umekopy na kupaste.

>>Biblia inasema tuende kwa hekima na walio nje, kumbuka hili kumtumikia Mungu kusikuondoe kwenye uwepo wa Bwana. Nikihitaji kuja kufundisha huwa naenda kwanza uweponi mwa Bwana na siendi kwenye biblia kwanza. Maana Biblia inasema laiti wangelikaa barazani Pangu walingewasikilizisha watu wangu maneno yangu. Uweponi mwa Bwana ndio utakuongoza uende wapi kwenye biblia na kwa mtirirko upi ili uweze kuwasikiliza watu maneno yake.

>> Mwaka Fulani niliota ndoto, Mungu aliponisemesha kuomba maombi ya kifalme. Na shetani alinipiga vita sana, Yesu alikuja na Malaika na wakapigana sana na shetani na wakashinda ie vita. Mara nikamuona Yesu akiondoka nikamsemesha kwa kiingereza kuwa ‘’*Jesus I thank you* akawa anaenda tu wala harudi, nikamsemesha tena akageuka lakini akawa anaenda. Nipogeuza na kusema 8Jesus I worship you* akasimama na nikamsemesha tena na tena aakanza kuja pole nilipokuwa.

>>Baada ya hapo Mungu alinifundisha kitu kikubwa sana kuwa kumwabudu Mungu kunamfanya Mungu akae hapo na mimi nikaanza kusoma upya habari za kuabudu kwenye biblia na nimejifunza mambo mengi sana na nazidi kujifunza mpaka leo

>>>>Baada ya hapo tuliomba sana kukabidhi kwa Mungu kila kitu kinachotuzuia kutomwabudu.

Endelea kutufuatilia Gospel kitaa kwa muendelezo wa Mafundisho.

*Felix*…
www.facebook.com/felixmbwanji

*Semina hii pia iko live Youtube kwa link hii Kuanzia saa kumi jion na recorded zipo * https://www.youtube.com/channel/UC4p4lrpgpNd-9bHPgHJ4xWw na *Ustream* http://www.ustream.tv/channel/mwakasegemanaministry

Share on Google Plus

About John Maulid

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.