SOMO: KOMBOA LANGO LA MUDA WAKO ILI UPATE ULICHOPOTEZA

*NA MWL CHRISTOPHER E.A.  MWAKASEGE*

*TAREHE 9 SEPT 2016*.

*SIKU YA 6*

*KOMBOA LANGO LA MUDA WAKO ILI UPATE ULICHOPOTEZA*

Haleluya haleluya …….. keti taratibu kwenye uwepo wa Bwana. Leo ni siku ya sita na tumesogea kidogo, na sina namna ya kuweza kurudi nyuma na kama hukuwepo jitahidi pata kanda sikiliza na kusikiliza. Huwezi pata mambo yote kwa dakika chache. Sikiliza na kusikiliza. Namna ya kupata kanda za mafundisho tembelea www. mwakasege.org utapata maelezo mazuri namna ya kupata kanda hata kama uko mbali.

Fungua na mimi KITABU cha *Waefeso 5:15-17* _ ‘’Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; *MKIUKOMBOA WAKATI KWA MAANA ZAMANI HIZI NI ZA UOVU*. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana’’_

~~Lengo la somo hili ni kuwa ukomboe wakati uliopo ili ukufanye utembee katika mapenzi ya Mungu. Kuna vitu Mungu aliumba kwa ajili ya kubeba muda. Na tuliangalia *Fikra, sheria na muda wa kuabudu* Leo nataka kuendelea ndani kidogo na tuangalie suala..

*MUDA WAKO WA KULELEWA*

*Ufunuo 12:1-5*   _Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili. Naye alikuwa ana *mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa*_
_Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba. Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake. *Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi*_

~~Tunaona picha ya mtoto aliyekuwa tayari kuzaliwa  na mama yake alipokuwa anamzaa shetani alikuwa ajitegesha ili aweze kumlea maana shetani alikuwa hana mpango wa kumuua.  Katika Lugha ya kiingereza wametumia neno la kulea kwa maana kulea kwa uharibifu . Nia ya kulea ni uzuri ila kwa mnatiki ya hapa shetani anaka kulea kwa uharibufu.
~~Mungu hakutaka yule mtoto alelewe na shetani na ndio maana alimnyakua na kumpeleka juu mbinguni.

*1* *Kuzaliwa kunaachilia lango la muda lililofunguka ili kuingiza kilichozaliwa katika mfano Fulani wa maisha.*

*Yohana 3:3-5*  _Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Nikodemo akamwambia, *Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa*? Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu_

*Wakolosai 1:13-14* _Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote_

~~ *Ukiona kitu kimezaliwa ina maana kuna lango la muda linakuwa limefunguliwa* Yesu alizungumza na Nikodemu habari za kuzaliwa mara ya pili na alieleza yafuatayo
*1*Kuona ufalme wa Mungu.
*2* Kuingia ufalme wa Mungu.
~~Hizi ni sentensi mbili tofauti kabisa. Sasa katika hali ya kawaida tuliyoizoea kuwa kuzaliwa mara ya *pili kuokoka* na huwezi kuingia ufalme wa Mungu kama hauna wokovu ndani yako, vivyo hivyo hata hali ya kumuona Mungu. Katika kitabu cha Wakolosai ni kuwa Yesu anatuhamisha toka ufalme wa giza na kutuleta katika ufalme wa mwana wa pendo lake.

~~Ufalme ni mfumo wa utawala  ambao unahusika ili kutengeza aina Fulani ya maisha ya watu ili waweze kuishi katika mfumo huo. Kwa hiyo lengo la kuzaliwa katika mfumo Fulani wa maisha ni ili mtu alizaliwa hapo awezze kuwa chini ya huo mfumo.

~~Kwa mfano wewe ni Mtanzania na umezaliwa Tanzania, hapo utakuwa chini ya ufalme wa Kitanzania na huo ndio unakuwa mfumo Fulani wa maisha.

*2*  *Lengo kubwa la malezi ni kumuandaa mtu kimaisha kwa msingi wa muda.*

~~Bibia inasema kuwa shetani alikwa anataka mtoto aweze kulelewa na Yeye ili apate nafasi ya kuweza kupandikiza vitu vibaya na mwisho wa siku awe mtumishi wa Ibilisi. Mithali 22:6 ‘’ Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

~~Kazi ya malezi ni maandalizi ya msingi ili upande vitu kwa mtoto na uweze vitumia katika hali yake ya akiwa mzee.  Shetani alikuwa anataka kuweka kuweka mfumo Fulani wa maisha yake ili aweze kumzuia kutembea katika mapenzi ya Mungu.

*3* *Kuna tofauti ya umri wa kiroho na mtu wa umri wa kimwili wa mtu*

*Mfano*
*Zaburi 103:5* ```Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai```; huu mstari una vitu vikubwa sana. Kwa kiumri ni mzeee ila kiroho ni kijana.  Lakini ukiangalia *Wagalatia 4:1-2*  _Lakini nasema ya kuwa mrithi, *wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa*, angawa ni bwana wa yote;  bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba_ 

~~Wakati wowote awapo mtoto ni sawa na mtumwa yaani anakuwa hana maamuzi yoyote. Bali ukienda kusoma *Yohana 3:4* Nikodemu aliuliza ya kuwa awezaje mtu kuzaliwa akiwa mzee? Swali hili Nikodemu aliuliza kwa sababu Fikra zake zilikuwa hazijui kutafsiri kiroho bali yeye alikuwa anafsiri kimwili na alishindwa kutafakari kiroho maana katika zaburi tunaona ya kuwa ujana wa mtu unarejeshwa hata kama akiwa mzee

*4* *Muda wa Kiroho wa mtu ndio unaongoza aina ya maisha ya mtu*
     *Mithali 22:6* *Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee* na  *Zaburi 103:5* ```Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai```;

~~Katika ulimwengu wa Roho kuna vipindi hivi.
~~~~Utoto ni muda
~~~~Ujana ni muda
~~~~Uzee ni muda

~~Ndio maana ukivuka kutoka kwenye muda wa ujana na kwenda kwenye muda mwingine ujue kuwa kuna lango unakuwa umefungua. Muda ni lango *Mwanzo 8:21* biblia inasema *tangia ujana mawazo ya mwanadamu ni maovu*  bali katika *1Wafalme 18:12* biblia inasema mtumishi huyu alikuwa na *hofu ya Mungu tangia ujana* wake. Katika kitabu cha mwanzo tunaona ya kuwa mawazo mabaya yaliingia katika hatua ya ujana, pia katika wafalme tunaona hofu ya Mungu iliingia katika huu ujana wake. Angalia tena Wagalatia 4:1-3, biblia inasema kuwa mtu hata kama ana miaka mingi lakini kiroho akiwa bado ni mtoto basi bado ataoneakana ni mtumwa hata kama ni mrithi. Na haya mambo ni ya kifikra Zaidi maana mtu anaweza akawa na miaka mingi lakini fikra zake bado akaonekana kama ni mtoto kwa sababu fikra zake hazijakaa sawa yaani hajakua kifikra.

*5* *Aina ya muda wa kiroho na za kimwili zinazomhusu mtu zinaweza kumsumbua mtu kimaisha*
*Yeremia 1:4-8*  Mungu alimwambia Yeremia kuwa kabla hajamuumba alimjua na alimuweka kuwa nabii wa mataifa lakini bado Yeremia alikuwa anajitetea kuwa yeye ni mtoto. Na ndani yake iliingia hofu alipokuwa anataka kulinganisha aina ya wito ambao Mungu alimutia na aina ya umri wake.

*Waamuzi 6:14-15* Tunaona habari za Gideoni na Malaika alipomfuata na kumwambia yeye ni shujaa ona alichosema nae alianza kujitetea kuwa yeye ni masikini sana na yeye ni mdogo katika nyumba ya baba yake. Na hofu ilimuingia.

~~Muda wa kiroho ndio unabeba upako juu ya kipindi kile na ukinyang’anywa huo muda na ukatekwa ina maana unakuwa umebanwa mahali Fulani. Angalia tena *Zaburi 103:5* ```Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai```; kwa maana hiyo Mungu akikuokoa anakurejea tena ule muda uliopoteza hata kama ukiwa mzee kiroho bado utakuwa kijana

~~Huyu ni mzee na Mungu ameweza kumpa tena ujana wake. Ndio maana unaweza kuta mtu anapokuwa mzee akili zake zinaanza kuwa sharp kuliko za kijana, na mara kidogo anaambiwa anastaafu. Na lile neno kustaafu hata kwenye biblia halipo na ona kinachotokea hata kama alikuwa sharp kwa kuwa amesikia kustaafu akili yake inaanza kushut down pole pole na mwisho hata mwili wake unashutdown kwa sababu ya taarifa hiyo aliyoipeleka kwenye mwili wake. Na wastaafu wengi sana huwa wanakufa, kwa sababu ya kuweka fikra ndani yao zinazowaua pole pole *(neno kustaafu kukaa ndani yao)*

~~Haijalishi kama una miaka mingapi sema nabadilisha kazi sio kwamba unastaafu maana Mungu anakurejeshea tena ujana wako. Huwaga nawauliza sana watu wanaokuja kwangu na kuniambia niwaombee baada ya kustaafu, na huwaga nawauliza sasa mtakwenda wapi, atasema nataka nifanye biashara, na mimi huwa nawauliza je umefanya kazi kwa miaka mingapi ataniambia miaka 40 au 30. Sasa Fikra zako zimezoea kupangiwa kazi na unakata ufanye biashara huana hata uzoefu nao, basi uwe na uhakika kuwa hizo hela zitapotea maana fikra zako hazijalelewa kufanya biashara. Kabla ya kustaafu anza kujipanga mapema pole pole. Au basi mtafute mtu mzoefu kwenye biashara ili aweze kukulea pole pole

*6* *Unaweza kulelewa tofauti na kile ambacho Mungu kakukusudia katika maisha yako*
*Yeremia 29:11*  _Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho_

~~Mungu anatuwazia mawazo mema ya kutupa tumaini siku za mwisho katika kiingereza ndio wameandika vizuri sana maana bibia inasema *to give you hope and future* . Mungu anataka kutupa tumaini na maisha mengine lakini haya yote yanaambatana na muda wa kiroho.

*Waefeso 1:3,4,5*   Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo; *```kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu```* watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.

~~Mungu alitangulia kutuchagua tangia awali  na alitufanya watakatifu wake, ina maana tulipozaliwa Mungu alituingiza katika system Fulani ya maisha. Kama Mungu alilitengeneza koo lako litoe sauti nzuri na kuwa na tune nzuri ina maana Mungu anataka uitumie katika kumwimbia Yeye, lakini cheki shetani akiwahi na akakupeleka kwenye bolingo bolingo na ona tune na sauti yako nzuri inaenda kwenye kuimba bolingo bolingo na huko unakuwa unaimba vizuri na kupata mashabiki wengi

~~Hata kama uko Misri basi usikae huko maana biblia inasema tokea Misri nalimuita mwanangu. Sijui uko wapi, ikifika saa ya Mungu kukuita ni lazima atakutoa huko Misri ili akurejeshe kwake na ukamtumikie. Haleluyaaa haleluyaaa!!!!!!!

*Wagalatia 1:13-16* ```Maana mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu. Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu.
Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake, alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu```

~~Biblia inatuambia kuwa Paulo alipozaliwa lilifunguliwa lango lingine kutokana na aina ya malezi aliyolelewa. Maana alililewa kwenye mazingira ya dini , japo yeye alikuwa ni mhubiri wa injili.  Na fahamu hili mtu akiwa yuko hospital na anacheki Afya ya mapafu yake kuingia na kutoka kwa oxygen unaona katika ile mashine kunakuwa kunacheza cheza yaani kuna mstari unaonesha kuwa hewa inaingia na kutoka ila ukifa sasa, mstari ule unakuwa flati yaani hausomi chochote. Hii ndivyo yalivyo maisha ya mtu aliyekufa kiroho muda wake unakuwa uko flati. Lakini ukizaliwa mara ya pili unafufuka kabisa.

~~Wana wa Israel walipotoka Misri  Mungu alisema huu ndio mwanzo kwenu, yaani kwenye ile miaka 430 waliyokaa Misri kama kwa mshale wa kimungu wa muda ulikuwa umesimama yaani uko flati. Lakini walipoondoka, Mungu alitenda jambo kwao na kuwaambia huu ndio mwanzo kwenu. Na alinza kuhesabu sasa

~~Yesu alipozaliwa Herode alimuwinda na alikuwa anataka kumuua na akakimbilia Misri, lakini saa ile Mungu akamuita toka Misri nae akaondoka Misri na kurudi tena katika ile nchi yake ili akalitumikie kusudi la Bwana.  Hata kama umelelewa misri basi usiendelee kukaa Misri ondoka Mungu anapokuita na ukiitika kuna lango jipya Mungu atalifungua kwako.

~~Musa alipozaliwa  alipata tabu kidogo katika malezi yake maana ni sawa alinyonyeshwa na mama Yake lakini alilelewa na Farao. Maana biblia inasema enyi wababa waleeti watoto *Waefeso 6:4*  Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; *bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana* . Unaweza mnyonyesha mtoto lakini usimlee maana wababa ndio jukumu lao kuwalea watoto.  Sasa Musa alilelewa na Farao lakini ukisoma Waebrania biblia inasema musa alisema kuwa si vema kujifurahisha na dhambi kwa kitambo akaamua kuondoka kwa Farao.

~~Huwa nikisoma habari za Rahabu huwa najiuliza sana kwanini Mungu aliiingi gharama sana ya kuweza kuibomoa Yeriko wakati alikuwa haitaki. Maana Baada ya kuibomoa  Mungu alimwambia Joshua kuwa ailaani Yeriko. Lakini ona  Mungu aliingia gharama ya kumtuma Malaika ili awepe ramani ya namna ya kuivamia Yeriko na pia waliizunguka Yeriko mara saba. Lengo lilikuwa ni moja tu *Rahabu*

~~Japo Rahabu alikuwa na Imani lakini shetani alikuwa amemzuia na ukuta maana Rahabu alikuwa ni mtu wa muhimu sana katika ukoo wa Yesu angalia Mathayo 1;5 utamuona huyu mama katika ukoo wa Yesu. Saa ya Rahabu ilipofika Mungu aliingilia kati mji mzima na kuubomoa kabisa na kumuokoa mtu mmoja tu na ndugu zake. Na Rahabu alisema na ndugu zangu nao waokoke maana yake hata kama ni wewe Mungu anakuokoa anaweza okaoa hata ndugu zako. Maana kuokoka kwako wewe kutakuwa ni msaada sana kwa ndugu zako na watu wengine na dunia nzima.

~~Sijajua shetani alikuwahi kwenye malezi yako na akabadilisha maisha yako wa utoto wako, lakini yupo Yesu anayeweza geuza kabisa mambo yako na kukuwafanya uwe mtu wa tofauti kabisa. Maana atakuhamisha na kukuingiza katika ufalme wake, na ndio maana haijalishi umeokoka lini au una watoto jizoeze kumuomba Mungu akulee mwenyewe maana biblia inasema watoto wako watalelewa na Bwana.

~~Mtu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Bwana. Na basi jizoeze kulisoma neno la Mungu na kulila maana kadri hiyo utaendelea kukua na kukua na Mungu atakusaidia. Leo unaposikia sauti ya Mungu kukuita usifanye moyo wako kuwa mgumu. Rudi kwa Bwana ali aweze kukupa lango jipya la muda wako.

*Baada ya hapo watu maelfu walikuja kuokoka na Mwl  Mwakasege aliwaongoza Sala ya toba na wakampokea Yesu*

Hata kama ni wewe hujaokoka basi leo fanya uamuzi huu wa kuokoka na Yesu awe ni Bwana kwako. Warumi 10:9 mkiri Yesu na aanza kushirikiana na watu waliokoka.

Barikiwa sana na tuonane tena katika sehemu ya 7 ya semina hii. Zidi kuomba Mungu azidi kufanya makuu kwenye semina pia na kwa watumishi wake kwa njia mbali mbali.

Endelea kutufuatilia Gospel Kitaa kwa Muendelezo wa Mafundisho

*Ubarikiwe na Mungu*

Pia iko live Youtube kwa link hii https://www.youtube.com/channel/UC4p4lrpgpNd-9bHPgHJ4xWw na Ustream http://www.ustream. tv/channel/mwakasegemanaministry
🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻

Share on Google Plus

About John Maulid

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.