SOMO: KOMBOA LANGO LA MUDA WAKO ILI UPATE ULICHOPOTEZA

*NA MWL CHRISTOPHER E.A.  MWAKASEGE*

*TAREHE 10 SEPT 2016*.

*SIKU YA 7*

*KOMBOA LANGO LA MUDA WAKO ILI UPATE ULICHOPOTEZA*

Bwana Yesu asifiwe, leo upako ulio juu yangu sio ule wa kufundisha watu wengi kama hawa bali ni ule upako ambao Yesu alikuwa anakaa nao faragha yaani vitu vya ndani sana. Unahitaji sana kuenda nami ili uweze kuelewa maandiko haya.  Maana kuna masomo Yesu alifundisha hekaluni ni tofauti aliyofundisha katikati makutano na ni tofauti na yale aliyowafundisha wanafunzi hata katika kundi la wanafunzi bado alikuwa na wanafunzi watatu ambao nao aliwafundisha mambo yao. Leo naona kama mtu mmoja mmoja na sio kundi kama tulivyo hivi bali ni  tu mmoja mmoja laiyepo hapa.

~~Jana tuliangalia kuwa muda wako wa kulelewa ukitekwa, shetani atapisha hapo vitu vyake na ataharibu muda wako kabisa. Muda wa malezi ni muda muhimu sana kwako maana hapo ndipo mambo mengi huwa yanapandwa hapo.

~~Jana nilipata nafasi ya watu wanaotufuatilia kwa njia mbali mbali na kutuuliza maswali. Na leo nataka nijibu swali moja ambalo nilipata nafasi ya kusoma (Wauliza maswali huwa wanatuma kwenye namba zetu za simu na katika ukurasa wetu wa facebook.

*UTAJUAJE YA KUWA UMEPOTEZA AINA FULANI YA MAISHA KUTOKANA NA MALEZI ULIYOYAPATA*
*Daniel 1:3-6,19*  _‘’ Mfalme akamwambia Ashpenazi, mkuu wa matowashi wake, awalete baadhi ya wana wa Israeli, wa uzao wa kifalme, na wa uzao wa kiungwana; vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao_
_Huyo mfalme akawaagizia posho ya chakula cha mfalme, na ya divai aliyokunywa, akaagiza walishwe hivyo muda wa miaka mitatu; ili kwamba hatimaye wasimame mbele ya mfalme. Basi katika hao walikuwapo baadhi ya wana wa Yuda, Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria_

19 _Naye mfalme akazungumza nao; na *miongoni mwao wote hawakuonekana waliokuwa kama Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria*; kwa hiyo wakasimama mbele ya mfalme_

~~Mara nyingi tunaangalia habari hizi kwa Daniel na marafiki zake  na leo nataka tuangalie kutoka kwa hao ambao hawajapata kazi. Na hatujajua walikuwa ni wangapi lakini tunaona kati yao walipata kazi watu wanne tu. Ukisoma maandiko vizuri utaona ya kuwa shule hiyo waliyokuwa wamesoma ilikuwa ni kwa muda wa miaka mitatu. Yaani kwa wakati huu tunaweza ita ni *degree*

~~Ni kweli elimu haina mwisho ila maarifa yanafungwa na muda.  Akina Daniel na wenzake walikuwa wanaandaliwa ili kuja kufanya kazi katika Ikulu ya mfalme wa Babeli.  Na Baada ya miaka mitatu ya kusoma kwao waliopata ajira *walikuwa ni wanne tu* sasa jiulize wengine wako wapi maana elimu waliyoipata na sijui wataitumia wapi. Maana kusoma kwao miaka mitatu inakuwa ni bure kabisa.

~~Swali ninalojiuliza ni kwanini Nebukadreza alikubali kuingia gharama ya *kuwalipia full scholarship* watu wote hao na wakati yeye alikuwa anahitaji watu wanne tu. Na kama alikuwa anahitaji watu wanne tu kwanini sasa asingewachukua hao wanne tu na kuwasomesha hao. Na kwanini aliweka mtihani wakati angeweza wafundisha hadi wafikie maarifa aliyokuwa anayataka.

~~Mwalimu kazi yake ni kuwalea wanafunzi kifikra ili waweze kutumika katika kipindi watakochohitajika,. Sasa kazi ya Mwalimu akipewa miaka mitatu ya kuhakikisha kuwa unapata maarifa Fulani basi baada ya kipindi hicho kupita ina maana kuna Fikra unatakiwa uwe unazo baada ya muda huo. *Hawa vijana muda wao wa miaka mitatu ulipotea bure* maana baada ya kumaliza hamna mtu aliyekuwa anahitaji tena walichosomea.

~~Angalia walichofundishwa, walifundishwa Elimu ya Kikaldayo na lugha ya kikaldayo, maana elimu hii ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya wakaldayo tu na wasingeweza tumia mahali popote. Ndio maana ukiwa na maarifa ya kiingereza inatakiwa pia uwe na lugha ya kiingereza.  Maana ukiwa na maarifa ya kiingereza na hauna lugha ya kiingereza basi uwe na uhakika kuwa utakosa kazi.

~~Kama umelelewa vibaya na kile ulichopandikizwa ndani yako hakitumiki tena, au kikitumika unakitumia vibaya. *Hutafuti kazi baada ya kumaliza kusoma bali unatafuta kazi kabla ya kwenda kusoma* maana biblia inasema *anatangaza mwisho tangu mwanzo*.  Na ukianza kutafuta kazi baada ya kumaliza unakuwa unaendana tofauti na kanuni hii.

~~Hawa watu waliandaliwa kwanza kwa ajili ya kuja kusimama mbele ya Ikulu ya Nebukadreza na baada ya miaka mitatu hawakupata kazi. Na huwezi mlalamikia Nebukadreza kwa kutokukupa kazi maana kama ni kusoma ulienda kusoma wewe mwenyewe. Kumbuka hili *Elimu haikupi kazi bali maarifa ndiyo yanakupa kazi.*

~~Mungu anapokuandaa katika kipindi Fulani ina maana kuna maarifa anataka uwe nayo ili yaje yakusaidie. Sasa chukulia umeenda chuo Fulani kusoma na baada ya kusoma miaka mitatu na hauna kazi, basi chuo hicho hicho kikitangaza nafasi za masomo basi uwe na uhakika wadogo zako hawatenda kusoma maana hutataka na wao wapoteze mud kama na wewe ulivyopoteza.

~~ *Ni rahisi kuzuia muda wako wa malezi kupotea kuliko kuukomboa ukipotea* . Vitu walivyokuwa navyo ilikuwa ni vigezo vya kupata chuo na sio kazi , na kama ni elimu walikuwa nayo lakini ilinyongwa kipindi cha malezi.  ( _Daniel 1:4 vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, *wenye kufahamu elimu* watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme.  Tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao_ ) lakini elimu zao ziliuwawa na elimu ya Nebukadreza aliyotaka wapewe kwa miaka 3 .

~~Nilikuwa mkoa mmoja nilikuwa nafundisha habari za elimu, na watoto wa eneo lile wanamaliza elimu ya msingi na hawana maarifa ya msingi ya kuweza wasaidia katika umri walionao. Na ni sawa na watu wanaomaliza chuo kikuu na hawana maarifa ya kuwasaidia katika maisha yao. Ni kweli elimu wanayo ila haiwasaidii.  Maana unaweza ukasomea kozi na usipate kazi. Si kwamba kazi hakuna ila ni kuwa maarifa yako hayahitajiki au yamepitwa na wakati au maarifa yako ni mbele sana kwa hiyo hadi tupate nafasi za kazi inahitaji muda kidogo.

Sasa twende kwenye Ufunuo 12:4 Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, *amle mtoto wake*.

~~Hapa nataka nikufundishe vitu vya ndani kidogo ambavyo unavipata ukiwa na fellowship na Yesu. Kuna tofauti kati ya kulisema neno kabla hujasoma na baada ya kulisoma na ndipo unalitamka. Ukitamka bila kulisoma moja kwa moja utatamka *amle* lakini ukilisoma neno hili alafuta ndio ulisome utaona kuwa ni *amlee*. 

~~Sasa ukimtaka neno *amle* unakuwa umepoteza kitu kikubwa sana. Twende kwanza kwenye *Mathayo 13:13-14* *```Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa. Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona```*
~~Kwa hiyo katika biblia si kila anaesoma neno anaona  na si kila anaesikia neno la Mungu anasikia. Hapa ndipo shetani anawapiga sana chenga watu. Sasa ukitaza kusikia maana yake sikia na kusikia ndipo utasikia na kuelewa na neno litazaa kile kinachotakiwa uzae kupitia hilo neno.

*Mathayo 13:18-19,25*  _Basi ninyi sikilizeni mfano wa mpanzi. *Kila mtu alisikiapo neno la ufalme asielewe nalo, huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake*. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia. lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake._

~~Umeona yaani neno la ufalme usipoelewana nalo shetani anakuja kupanda magugu. Na lengo lake ni kuwa kile unachokisikia usije ukakielewa kwa sababu neno ni mbegu na mbegu inakuwa na muda ndani yake na shetani akikuzuia usielewe neno la ufalme unakuwa unakosa kitu kikubwa sana.

~~Angalia *Luka 24:44-47*  _Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. *Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko*. Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya. Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu_

~~ Kwa miaka 3 walikuwa wanamsikia akifundisha na hawakumelewa na walikuja kuelewa baada ya kuwafunulia akili zao ili weweze kuelewa maandiko Angalia tena *Mathayo 133:16-17* _Lakini, heri macho yenu, kwa kuwa yanaona; na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia. Kwa maana, amin, nawaambia, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi, wasiyasikie_

~~Maana ya mistari hii ni kuwa *1* *_walitamani kuishi kipindi chenu hiki_ *  *2* * _Kati Yenu wapo manabii na wanatamani kusikia kama nyie mnavyosikia lakini hiyo neema imewapita mbali_*

~~Biblia inasema heri kwa kiingereza neno heri maana yake ni *blessed, na maana ya blessed ni  to be empowered*  Siku moja nilikuwa eneo Fulani na mhubiri mmoja alihubiri jambo Fulani na mimi nilisikia na nilipowauliza wao kama wamesikia nilichosikia mimi, lakini wao walikuwa hawajasikia.  _Ufunuo 12:4 ‘’4Its tail swept athird of the stars out of the sky and flung them tothe earth. The dragon stood in front of the woman who was about to give birth, *so that it mightdevour her child the moment he was born*_

_Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili. Naye alikuwa ana *mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa*_

~~Katika kiingereza wametumia neno *devour* maana yake ni *be totally absorbed by powerful feelings* sasa twende kwenye _1Petro 5:8 ‘’ Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, *akitafuta mtu ammeze*_  sasa cheki kwenye kiingereza _Be alert and of sober mind. Your enemy the devil prowls around like a roaring lion lookingfor *someone to devour*_

~~Katika mistari hii yote utaona ya kuwa wametumia neno *Devour* kwenye neno *ammeze* na *amle*. Tufika mpaka hapo, ukiona nakuacha rudi tena hapo juu maana ya devour ili twende kwa pamoja.

*Habakuki 1:13* _‘’ Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu *ammezapo* mtu aliye mwenye haki kuliko yeye;_  angalia sasa kwenye kiingereza *’’swallow up those more righteous than themselves?”*

*Habakuki 3:14* _Ukakichoma kichwa cha mashujaa wake kwa fimbo zao wenyewe; Wakaja kama kisulisuli ili kunitawanya; *Kama wakifurahi kuwameza maskini kwa siri*_angalia na kiingereza chake _14 With his own spear you pierced his headwhen his warriors stormed out toscatter us,gloating as though *about to devourthe* wretched who were in hiding

~~Hapa tunaona neno devour limetumika na mstari wa 13 neno swallow ndilo limetumika . sasa kumeza kwa hali ya kiroho sio kuondoa tu uhai bali ni kubana kitu kiroho ili kisikae sawa. Sasa shetani alipokuwa anapambana na Yesu kwa ngazi ya kiroho baada ya kutaka kumkimbiza Yusufu ili Mariamu auawe kwa sababu wangesema huyu mwanamke kapataje hii mimba maana kwa sheria za wakati ile mtu akipata mimba nje ya ndoa ilikuwa ni kuuawa. Akajaribu tena kumtumia Herode lakini lako alishindwa.

~~Sasa sikia biblia inasema Roho Mtakatifu alimpeleka Yesu Jangwani ili kujaribiwa na shetani. Na ona shetani alichofanya akasema Yesu amsujudie  na kama alikuwa na shida ya kumuua kwanini asingemuua na alisema anataka amsujudie. Lengo la shetani alikuwa anataka Yesu amtumie kwenye kusudi lake. 

~~ *Yoeli 1:4* _Yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige; na yaliyosazwa na nzige yameliwa na parare; na yaliyosazwa na parare yameliwa na madumadu. Na cheki *Yoel 2:25* _ Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu._

~~Hapa tunaona hawa wadudu walikuwa hawali nafaka bali walikuwa *wanakula miaka* na ndivyo biblia inasema.  Na ndio maana Mungu alisema atarudisha miaka iliyoliwa na nzige  na sio nafaka.  Ukisoma *Kumbukumbu la Torati 30:19* _‘’ Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; *basi chagua uzima*, ili uwe hai, wewe na uzao wako_

~~Hapa Musa alikuwa anazungumza na watu waliohai kabisa na walikuwa hawajafa, lakini aliwaambia kuwa wachague uzima, maana yake walikuwa bado hawajaanza kuishi na ndio maana alisema chagua uzima  ili uwe hai. Shida ya neno la Mungu si kusoma au kusikia bali shida ni kupata kilichoko ndani na bila kusikia kilichoko ndani utakuwa umepoteza kitu kikubwa sana.

~~Wakati Mungu alipowapeleka wapelelezi aliwaonesha majitu, na lengo lake si kuwatisha wana wa Israel bali alikuwa anataka wajifunze kutafsiri mambo kwa jinsi nyingine.  Na walishindwa isipokuwa Joshua na Kalebu.  Na kama Mungu amekujalia neema hii ya kuja kutafsiri kwa namna nyingine basi heri yako.
~~ Ndio maana ukisoma Warumi 5:12-14 utaona kuwa baada ya dhambi kuingia mauti ilitawala, na mauti sio hali ya kifo bali ni mfumo wa maisha na ndio maana utawaona watu wanaishi lakini ndani yao wamekufa yaani mfumo wako wa maisha umevurugika kabisa.

~~*Hii ni Siri ngumu kidogo*, Shetani anajua kuwa ana muda mchache,eeeh si unakumbuka kipindi kile yale mapepo yaliposema kuwa unataka kututesa kabla ya wakati wetu?. Sasa sikia na yeye shetani hataki kuwaua wanadamu . ni ngumu eeeh. Ngoja nijaribu hivi kanuni ya kutembea kwenye ulimwengu huu ni lazima uwe na mwili na mwili huu kapewa mwanadamu tu. Mungu akitaka kuja duniani ni lazima awe na mwili na yeye ndiye anayeingia kwa mwandamu na malaika hawawezi ingia katika mwili wa mwanadamu maana Yesu tu ndiye anayeingia. Na shetani nae akitaka kufanya mambo yake hapa duniani atatumia mapepo ambayo yatawaingia wanadamu.

*HATUA ZA KUJUA KAMA MUDA WAKO UMETEKWA*
*1* *Mwombe Mungu abariki macho yako na masikio yako na itakusaidia kuona na vitu vingine ambavyo Mungu anataka uone* angalia Waefeso 1:17-23, jiombee hii sala wewe mwenyewe na utaona macho yako ya rohoni yakifunguka

~~Si mnakumbuka wale vijana wa Emausi, Yesu alikuwa pamoja nao njia nzima na hawakuweza kumtambua na ilipofika saa ya kumega mkate na alipobariki ule mkate na kuumega ndipo wakajua kuwa ni Yesu na saa hiyo akatoweka katikati yao. Oooh ni hasara sana kumtambua Yesu saa ndio anaondoka, na ona waliishia kujilaumu.

~~Kuna mahali unakuwa kwenye upako lakini watu hawamuoni Yesu na wanakuja muona Yesu saa ndio anaondoka. Unaposhiriki meza ya Bwana mwombe Mungu akufungue macho yako ya ndani ili uweze kuona.

~~ooh ukilijua hili Mungu ataingilia kati na Mungu atasema saa imefika sasa ya wewe mauti kumezwa na wewe na Mungu ataitowesha mauti na kukupa roho wa uzima na wewe utatembea katika uzima.. Haleluya haleluya… glory to God, Glory to God.

*2* *Omba Mungu akupe kujua thamani ya alichokuumbia*
~~Esau hakujua thamani ya mzaliwa wa kwanza hadi pale alipoona baada ya kuizua kwa Yokobo akajua kuwa amepoteza kitu kikubwa sana. Sasa unaupata wapi ujasiri wa kudharau kitu Mungu kakuumbia ndani yako na unategemea Baraka za Mungu zitoke wapi? Shetani ndiyo anataka ujidharau na akupoteze.

*3* *Omba Mungu akujulishe kama miaka yako imeliwa na nzige.

~~Mwingine anakata tamaa kabisa baada ya kupoteza muda wake, lakini namfahamu Mungu wangu ninayemuabudu kuwa anaweza rejesha yote yaliyoliwa na nzige. Hata kama uliona haiwezekani, Kwa Mungu hakuna jambo lisilowezekana.

~~Ilikuwa ni 1990 msichana mmoja alikuwa ananisimulia maisha yake kuwa baada ya kupata ujauzito alipokuwa sekondari na kupitia mahali pagumu sana na nyumbani kwao walimfukuza. Na akajifungua yule mtoto kwenye mazingira mabovu sana. Basi neema ya Mungu ilimjia na akaokoa na baada ya kuokoa akamuomba Mungu, kuwa Mungu je hapa ndipo uliponipangia niishie hapa?  Mungu akamletea picha yule msichana kuwa kasoma hadi chuo kikuu na anakazi nzuri.

~~Yule msichana akaomba Mungu amsaidie amrudishe tena shuleni na alisoma na alipokuwa ananisimulia wakati huo alikuwa tayari accountant mkubwa wa benki moja hapa nchini.  Angeweza kata tamaa kabisa lakini alijitia moyo kwa Bwana na Mungu akamsaidia. Upo upako hapa leo … Mungu anapokupa muda ni muda wa kujipanga, kwanini Mungu akupe tena muda ambao anajua utaupoteza tena.
~~Wana wa Israel walipotoka misri na kuwapeleka Kanani walipopitia changamoto kidogo tu walijikuta wakikumbuka masufuria ya nyama za Misri japo walikuwa Mungu alikuwa kawaambia huu ndio mwanzo wa muda kwenu. Hata kama shetani anataka kakupanda magugu kwako kama alivyokuwa kapanda kwa Rahabu ukahaba leo yuko Mungu atakaebomoa Yeriko yako na kukutoa huko na kukurudisha kwenye muda wako aliokupangia.

~~Usikae na Magugu kwako, mwambie Yesu yatoe maana yakiendelea yatakutesa sana, wengi sana wameokoka lakini bado wana magugu ndani yao na Misri imejaa sana, unahutaji kwenda mbele za Bwana ili akusaidie.

~~Paulo japo alikuwa ametengengwa tangu tumboni mwa mama yake, lakini alikulia kwenye mikono ya dini na aliona anafanya sawa maana kuna mistari ya torati aliyokuwa anatumia kuisimamia dini. Lakini alipokutana na Yesu na magamba kumtoka machoni mwake, mistari ile ile akaanza kuitumia kwenye kueneza injili ya Yesu.

~~Mimi mwenyewe miaka ile nazaliwa kabla nchi haijapata uhuru yule mzungu daktari kila mama alikuwa anamfanyia operation alikuwa anakufa mama pamoja na mtoto. Na mimi ndio nillikuwa nasubiri kuzaliwa na ndugu yangu mmoja nae alikuwa daktari na aliopoona ya kuwa yule mzungu kaondoka kwenda kwake akamhamisha mama kutoka kwenye wodi na akampeleka mahali pengine na akamfanyia mama operation na ndipo nikazaliwa. Mwingine atasema Mwakasege kazaliwa akiwa mtakatifu sana. Hapana haikuwa hivyo wazazi wangu walinilea katika hali ya kanisani na walikuwa wazee wa kanisa. Lakini shetani alitaka kunisumbua nilijifunza kwenda kwa waganga na kutumia hirizi. Nilikunywa kila aina ya pombe unayoifahamu. Nilifundishwa na marafiki zangu kuvuta sigara.  Lakini Yesu aliponiokoa maisha yangu yalibadilika jumla. Na hata marafiki zangu wengine wanashindwa kuamini kama ni mimi yule wa kipindi kile. Na kuna marafiki zangu wengine wamekufa lakini mimi niko hai na ni kwa neema tu ya Mungu.

~~Jifunze kwenda mbele za Bwana ili akukung’ute mavumbi yako fanya hivyo kila mara, na mimi huwa naomba Mungu anisaidie.

Baada ya hapo mwalimu aliomba kwa watu wote ambao wamefuungwa na nguvu za giza *’’akina Yusufu walioko magerezani’’* maana kuna watu shetani kawafunga. Nguvu za Mungu kubwa zana zilitufikia sana pale uwanjani tembela link hizi kuweza kuona namna semina ilivyokuwa na pia semina iko live kuanzia saa kumi.  https://www.youtube.com/channel/UC4p4lrpgpNd-9bHPgHJ4xWw  na Ustream http://www.ustream.tv/channel/mwakasegemanaministry pia ili kuweza kupata kanda za semina hii tembelea www.mwakasege.org

Endelea kutufuatilia Gospel Kitaa kwa muendelezo wa Mafundisho

Barikiwa sana na tuonane tena katika sehemu ya nane ya semina hii. Ubarikiwe na Yesu

Share on Google Plus

About John Maulid

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.