SOMO: KOMBOA LANGO LA MUDA WAKO ILI UPATE ULICHOPOTEZA *3

*NA MWL CHRISTOPHER E.A.  MWAKASEGE*
*TAREHE 6 SEPT 2016*.
*SIKU YA 3*
*KOMBOA LANGO LA MUDA WAKO ILI UPATE ULICHOPOTEZA*
*SUMMARY*
Bwana Yesu afiwe, leo ni siku yetu kama ni siku ya kwanza unahudhiria semina hii tumekwenda mbali kidogo. Sina namna ya kurudi nyuma ila jitahidi upande kanda za kuanzia siku ya kwanza. Sikiliza na kusikiliza, hata kama ulikuwepo huwezi daka chote kwa muda mmoja, chukua cd sikiliza tena na tena.
_Waefeso 5:15-17 ‘’ Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; *MKIUKOMBOA WAKATI KWA MAANA ZAMANI HIZI NI ZA UOVU*. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana’’._
>>Muda umepewa jukumu kubwa sana kubeba maisha ya mtu, na ukitaka kufupisha maisha ya mtu unatumia unafupisha muda wa huyo mtu.
                                  *VIBEBEO VYA MUDA*
>>Jana tuliangalia kibebeo cha kwanza cha muda ambacho ni *FIKRA* na leo nataka tuangalie kibebeo cha pili
*SHERIA*
Daniel 7:25 ‘’ _Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; *naye ataazimu kubadili majira na sheria*; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.’’_
*JAMBO LA 1* *Uimara wa hali watakatifu kusimamia kusudi la Mungu, unategemea muda uliobebwa na sheria inayotumika wakati huo.
*Waefeso 1:3-4* Kwa mujibu wa mstari huu wa waefeso ni kuwa mtakatifu ni Zaidi ya kutokuwa na dhambi.
Paulo anasema alitengwa tangu tumboni mwa mama yake, na kutengwa ina maana ya kuset aside kwa kusudi Fulani la Mungu.
Ile Muungu kukuleta hapa duniani ina maana kunakuwa na kusudi la kazi Fulani ambayo anakuwa kakuleta hapa duniani.  Na kusudi maana yake ni sababu ya kuwepo. Ukisoma Mhubiri 3:1b biblia inasema *kuwa kila jambo lina wakati wake na kusudi chini ya mbingu*. Maana yake ni kuwa kila kitu uwepo wake unakuwa umefungwa na kusudi maalamu ambalo Mungu kapanga.
*Matendo ya mitume 13:36* Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia *shauri la Mungu katika kizazi chake*, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu. Daudi alikuwa tayari kalitumikia kusudi la Mungu wake kwa kizazi chake. Shauri maana yake ni kusudi yaani lengo la Mungu wake naye akalala.
Kwa maana hiyo hali ya utakatifu ni Zaidi ya kutokuwa na dhambi na ndio maana biblia inatuambia kuwa Mungu alimtenga Yeremia tangu akiwa tumboni mwa mama yake .Mungu akitaka utembee kwenye kusudi lake ina maana atakuzuia kufanya kitu kilicho nje ya kusudi lake na damu ya Yesu itasimama kama ukuta kukuzuia kutokufanya hilo jambo unalokusudia kulifanya. Na atahakikisha anaondoa fikra zozote ambazo zinataka kuingilia kati hilo kusudi la Mungu.
*JAMBO LA 2* *Majira na sheria yanapofanya kazi kwa pamoja vinakuwa ni uwanja wa mapambano ya kiroho na ya kimaisha,kati yako na waliotofauti na wewe kimisimamo au kifikra*
Wakolosai 4:5 ‘’ Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati.
Biblia inasema mwende kwa hekima kwa watu walionje ya kusudi au wale ulio nao tofauti kimisimamo ya Mungu. Na uwanja utakaokuwa unapambana nao ni uwanja wa wakati. Katika Daniel 7:25 shetani alikusudia kubadilisha majira na sheria ili aweze kuwadhoofisha watakatifu ili wasiweze kusimamia kusudi la Bwana.
>>Mungu hakupanga tuishi nae mbinguni milele bali alipanga tuishi nae hapa hapa duniani na ndio maana Yesu alisema naenda kuwandalia makao ina maana hayakuwepo na haya makao ni ya muda. Yahana aliona kuwa mji mpya Yerusalemu unashuka toka juu na aliona na nchi mpya kwa maana hiyo hii iliyopo inaondoka na hiyo mpya inakuja ili kuendeleza maisha ya wanadamu ambayo Mungu anakusudia kuwepo hapa duniani.
>>Suala la Roho Mtakakatifu kukusaidia kuishi hapa duniani, usijisahau sana kuwa unakuwa na mawazo tu ya kwenda mbinguni na tusahau namna bora ya kuishi hapa duniani. Maana shetani anatumia sana hio fursa ya watu kuwaza tu kwenda mbinguni na kusahau namna ya kuishi bora hapa duniani kwa nyakati hizi.
>>Sheria ni kibebeo cha muda na shetani anapobadili majira na sheria lengo lake ni kuwadhoofisha watakatifu ili wapoteze kuona umuhimu wa muda, majira na sheria.
>>Kwa mfano unaoa au unaolewa na mwenzio ina maana kila mtu anakuwa fikra zake na muda wake kwa hiyo mkiingia ndani ya ndoa kuna lango lingine la muda linafunguliwa na sheria mpya ya ndoa inakuwa inawafunga hakuna kutengana hadi kifo. Kwa hiyo msipokuwa makini kusaidiana kifikra yaani mwenzio akiwa pole pole na wewe hujui namna ya kumsaidia na yeye aweze kuchangamka unakuta na wewe unaanza kwenda kwa slow motion sawa na mwenzio. Na unaanza kusingizia shetani kumbe sababu kubwa ni Fikra zenu.
>>Hata katika hali ya kawaida watu wawilia au watatu wanakubaliana kufanya Biashara kwa pamoja alafu huku kila mtu anamuda wake na fikra zake, mwanzoni wataenda vizuri ila baada ya muda utaanza kuona wanaacha kuelewana  na mwisho wanakuja kuvunja hata hiyo biashara yao, na sababu kubwa ni kutokujua namna ya kuharmonize (kuweka sawa) Fikra zao ili waweze kutembea katika muda mmoja. Na hili jambo huwezi fanya tu ni hadi kwa msaada wa Roho Mtakatifu.  Pia huwa nawaambia sana Vijana kabla hawajaanzisha huduma wacheki kwanza sheria itakayokuwa inaongoza huduma yao maana wasipojua, itawasumbua sana kuendelea mbele.
*JAMBO LA 3* *Ukibadilisha sheria unabadilisha na wakati uliobeba aina Fulani ya wakati na maisha yanabadilika ili kuweza kuendana na sheria iliyobadilishwa*
>>Ikiwa sheria ikibadilika na muda usipobadilika kunaanza kuwa na ugumu wa kuendana pamoja na muda uliopo. Sheria inaweza kukusaidia uweze kuishi kwa muda ulioko au uliobadilishwa kutokana na sheria hiyo.
*JAMBO LA 4* *Sheria kuwa kibebeo cha muda kinaunganisha muda na maeneo mengine yafuatayo*
           a)Amri…Ordinance
           b) Hukumu..Judgement
           c) Agano… Covenant
           d) Agizo ….Decree
           e)Haki ….Justice
Haya maneno katika Lugha ya kiingereza yanakuwa na maana tofauti tofauti kwa kulingana na tafsiri ya Biblia kama ni King James, Amplified, NIV, NLT.etc
*Kazi ya Sheria ni kulinda aina Fulani ya maisha* Hukumu inazuia muda na ndio maana ukitokea mgogoro au ugomvi uwe na uhakika kuwa shetani anataka kakuiibia huo muda maana unakuta kila kitu kinastop.
*MFANO WA MABADILIKO YA MUDA NA SHERIA KATIKA KIPINDI CHA (HAMANI, MODERKAI, AHUSERO NA ESTA)*
*Sheria ya kwanza* *Esta 3:1-8* hapa tunaona kuingizwa kwa sheria inayotaka watu wote kumsujudia Hamani. Na hapa tunaona kuwa watu wanapokuwa kwenye taifa Fulani wanakuwa chini ya muda na sheria husika.  Hii sheria ya kumsujudia mtu wayahudi hawakuwa nayo na ndio maana Mordekai alikataa maana alijua mtu wa kumsujudia ni Mungu peke yake. Endapo angekubali kumsujudia Hamani tayari angekuwa anatembea kwenye muda mwingine.
*Sheria ya Pili* Esta 3:9-10 ‘’ Basi, mfalme akiona vema, na iandikwe kwamba waangamizwe; nami nitalipa talanta kumi elfu za fedha mikononi mwao watakaosimamia shughuli hiyo, waziweke katika hazina ya mfalme. Ndipo mfalme alipoivua pete yake mkononi, akampa Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi.
>>Sheria hii ilikuja na ilikuwa ni tarehe 13 December yaani mwezi Adari. Maana kwa wayahudi mwezi Adari ni mwezi wa 12 na lengo la sheria hii kuweza kuwabana akina Mordekai na wenzake.Sheria Yoyote huwa inaweka pressure juu ya muda wako.
*Sheria ya tatu* *Esta 4;9-11* Basi Hathaki akaja, akamwambia Esta maneno ya Mordekai. Ndipo Esta akasema na Hathaki, akamtuma tena kwa Mordeka. kusema, Watumwa wote wa mfalme wanajua sana, hata na watu wa majimbo ya mfalme, ya kwamba mtu ye yote, akiwa mwanamume au mwanamke, atakayemjia mfalme katika ua wa ndani, wala hakuitwa, *kuna sheria moja kwake*, ni kwamba auawe; isipokuwa yeye ambaye mfalme atamnyoshea fimbo ya dhahabu, ili aishi; wala mimi sikuitwa niingie kwa mfalme yapata siku thelathini.
>>Ukiangalia mstari wa 10 unaonaesha kuwa sheria hii ilikuja kumbana sana Esta na kumdhoofisha hali yake kabisa.  Na Lengo la Esta kuolewa ilikuwa ni kulisimamia  kusudia la Bwana , na kuolewa ilikuwa ni njia tu ili awepo mtu wa kiyahudi kwa wakati huo ili aweze kulisimamisha kusudi la Bwana. Upande wa pili wanayajua sana haya mambo (nguvu za giza) na huwa wanawahi sheria ili kuweza kuwabana watakatifu wasiweze kutembea juu ya muda ambao ndio unabeba kusudi la Bwana.
>>Hapo Esta alikuwa anasema si Suala la Kwenda kwa mfalme Ahusero bali ni sheria, na Esta alipokuwa anaomba maombi yafanyike ni ili yaweze kurejesha muda ili aweze kushughulika na sheria. Na asingeweza kushughulika na sheria ikiwa yuko nje ya muda. Kwa hiyo kurudishwa kwa muda wake yaani na ile position yake ingemsaidia kuweza kubadilisha sheria.
>>Ugomvi au mgogoro unapotokea unaua thamani ya muda katikati ya wagombanao. Maana vita hustopisha maendeleo maana watu watakuwa wanasema ngoja kwanza tumalize mgogoro ndipo tuendelee. Na kwa hali hiyo shetani anakuwa anakuibia muda wako na kuna mambo yake anayokuwa anayapitisha wakati ndio mnagombana na baada ya mgogoro kuisha unakuta kuna mambo mengi sana yamebadilika. 
*ZINGATIA HILI* *_Shetani anapokuletea ugomvi lengo lake ni kukuibia muda wako kuwa usahau mambo mengine. Na ukiona hali hiyo mwambie shetani kuwa hatapata huo muda wako na katikati ya vita beba bunduki na jembe pia, usiombee mgogoro au vita tu bali ombea na mambo mengine_*
Ukiibiwa muda unaibiwa na maisha pia.
*Warumi 8:1-2* *``` Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.```*
>>Mwekezaji akija kuwekeza haijalishi shida zetu zikoje mtalazimika kuzibadili tu ili aweze kuwekeza hapo kwenu.  Maombi ya Esta kwa Mungu yalikuwa ya kuomba, muda wake urudi na Mungu alirudisha sheria.
Yale maombi ya Esta yaligeuza kabisa maisha kwa wakati ule kuanzia tarehe ile ile ya 13 December, waandishi wale wale walioandika sheria ndio walele wale waliorekebisha na ile ile sheria iliyotaka kuwaua wayahudi iliwaua wale wale akina Hamani.
>>Kuna nguvu sana ya maombi hata katika kipindi cha Daniel maombi yake yalitunza sana muda wake na Mungu akamsaidia na Pia maombi ya Esta yalirudisha muda wake ukaruishwa.
>>Shetani alipokuwa anazuia maombi ya Daniel ili aweze kumdoofisha na siku 30 alikuwa anataka kupitisha baadhi ya mambo kwa spidi kubwa sana na ndio maana Daniel aling’ang’ana sana na Mungu na Mungu aliingilia kati sheria hiyo iliyokuwepo.
>>Wana wa Israel wangejua hii siri ya kujua namna ya kutangua sheria hizi wangerudishiwa na muda wao maana wangeomba kwa Mungu ili ashughulike na sheria hiyo na wasingekaa miaka 400 utumwani na wangeomba Mungu na Mungu angefupisha dhiki. Maana Mungu anafupisha muda na baada ya hapo dhiki inakoma.
>>Sijui unapitia sheria gani, au upo katika mazingira yapi,, Yuko Yesu atakayekusaidia na kukuvusha. Mlango wa Benki haufungwi na askari bali hufungwa na muda. Yaani ikifika saa kumi unafungwa na wanaandika *door closed* lakini kama una uhusiano na manager utampigia simu hata baada ya muda kupita na manager anamuambia askari afungue huo mlango hata kama muda umepita unaingia ndani
>>Yesu ni Zaidi ya manager wa benki na ukimuomba hata kama kuna sheria yeye yuko juu ya sheria na atakusaidia. Hata kama uko kwenye dhiki usigombane na dhiki bali shughulika na muda kwa sababu ukishughulika na muda maana utafupisha hiyo dhiki.
*Baada ya hapo tuliomba sana na Nguvu kubwa sana ya Mungu ilitushukia pale uwanjani. Barikiwa sana na Mungu*. Tembelea http://www.ustream.tv/channel/mwakasegemanaministry
Endelea kutufuatilia Gospel Kitaa kila siku kwa mafundisho yanayoendelea Jijini Arusha

Share on Google Plus

About John Maulid

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.