SOMO: KOMBOA LANGO LA MUDA WAKO ILI UPATE ULICHOPOTEZA


*NA MWL CHRISTOPHER E.A.  MWAKASEGE*

*TAREHE 8 SEPT 2016*.

*SIKU YA 5*

*KOMBOA LANGO LA MUDA WAKO ILI UPATE ULICHOPOTEZA*

*KUUNGANISHA IMANI YAKO NA KUMUABUDU MUNGU*

*Waefeso 5:15-17* _ ‘’Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; *MKIUKOMBOA WAKATI KWA MAANA ZAMANI HIZI NI ZA UOVU*. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana’’_

~~Nyakati hizi zimebeba aina Fulani za uovu na ndio maana inakuwa ni ngumu kutembea katika mapenzi ya Mungu. Tunahitaji muda wa Mungu ili kutusaidia kutembea katika nyakati hizi. Muda ni lango ya mwanadamu japokuwa Mungu anaishi kwenye hali ya umilele.

~~Baada ya kuangalia *Fikra, sheria na muda wa kuabudu* Leo tunakwenda ndani kidogo.

*Marko 7:6-9* _’’Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami; *Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu* ’’_

~~Umuhimu wa kuunganisha Imani yako na kuabudu kwako, maana pasipo hivyo itakuwa taabu sana kukutana na saa ya kuabudu ambayo Mungu habuduliwa kwa mujibu wa *Yohana 4:23*

~~Hakikisha unapata kanda za masomo haya na sikiliza na kusikiliza maana huwezi daka kila kitu kwa muda mmoja. Somo la kuabudu nimefundisha jana kwa lisaa limoja ivi, ila mimi Mungu alinifundisha kwa miaka kidogo kidogo.

~~Tunajua ya kuwa Imani  inakaa moyoni na kama kuna gap Fulani yaani ufa kati ya mdomo wako na moyo wako. Kwa maana hiyo mdomo wako utakuwa unamheshimu Mungu ila moyo wako haupo na kwa maana hiyo unakuwa unaabudu bure.

~~Inatakiwa upate faida kwa mujibu wa Warumi 12:1-2, kwa sababu ukiabudu kisawasawa Mungu ataingilia kati maisha yako na anabadilisha nia yako na kukutengeneza ndani yako ili uweze kutembea kwenye mapenzi yake.

~~Wakati Fulani Mungu alinikumbusha miaka ile kulikuwa na shida ya bidhaa nchini kipindi kile kuna vita ya Uganda. Kilikuwa ni kipindi cha kufunga mkanda maana kupata bidhaa za msingi kama mafuta, chumvi, sukari ilikuwa ni ngumu sana kupata. Na mimi nilikuwa *Afisa mipango na uthibiti Uchumi daraja la tatu* na nilikuwa nasimamia mafuta ya wilaya yote peke yangu.

~~Kwa Nyakati zile upatikanaji wa mafuta ulikuwa ni mgumu sana kiasi kwamba watu wakisikia kuna mafuta eneo Fulani ilikuwa ni foleni ndefu sana na wengine utakuta wamekaa masaa matatu, mawili kwenye foleni na wanaambiwa mafuta yameisha na wanarudi kwao bila mafuta ya vyombo vyao vya moto.

~~Mungu alinikumbusha jambo hili katika somo hili kuwa watu wengi wanaenda kanisani au kwenye mikutano mikubwa na vyombo vyao ili kupata mafuta ya Roho Mtakatifu na hawapati, walifikiri mchungaji au mhubiri atawamiminia mafuta lakini wanayakosa. Kama ni ibada tungesema wameabudu bure hawajapata faida yoyote.

~~Na kipindi kile nilipokuwa nafanya kazi na mtu mmoja alinijia ofisini akaniambia, kuwa unajua hizi lita za mafuta mnazotoa huwa hazinitoshi kabisa maana nahitaji lita kama 200 ivi ili ziweze nisaidia huko ninakokwenda kulima maana ni mbali kidogo. Baada ya hapo nikasikia Amani moyoni mwangu nikamwambia ntakupa. Na baada ya kumwambia hivyo alitoa hela nyingi kidogo na akaziweka mezani. Nikamuuliza hizi hela za nini, akasema wewe chukua tu hizi ni zako, nilimuelewa kitu alichokuwa anataka. Baada ya hapo nikasema chukua hela zako maana siwezi kukuuzia haki yako mafuta kama yapo ntakupa ila kuchukua hela yako hapana siwezi chukua.

~~Watu wengi wanajua kuwa kwa kutoa pesa nyingi basi watapata upako wa Roho Mtakatifu kutoka kwa watumishi. Lakini hawapati kwa sababu mwenye kutoa huo upako ni Roho Mtakatifu mwenyewe.

~~Hamna kitu kinachomsumbua Mungu  na anatapotafuta watu wa kumuabudu na asiwapate na bali anaona watu wanaosali tu. Biblia inasema hakuna kilichofichika mbele za Bwana. Sasa kwenye biblia tunaona kuwa Mungu anatafuta *watendakazi* maana watumishi ni wengi ila watenda kazi ni wachache, Mungu anatafuta watu wa *kumuabudu* na Mungu anatafuta *Kilichopotea*.

~~Mungu anapotafuta sio kwamba hawaonekani, bali ni kwa sababu ya vigezo vyake alivyojiwekea kumuabudu. Kumuabudu, kwenda kwenye madhabahu yake, kuokoka Mungu ni mwaliko *‘’Hakuna ajuae kwa baba bali amejaliwa’’* Ile Mungu kukuletea roho ya mwaliko ndani yako ina maana kuna kitu amekiona ndani yako.

*Yohana 8:31-38* , Hili kundi Yesu alilokuwa anaongea nao ni wayahudi waliomuamini kabisa, ule mstari wa 37 Bilia inasema ya kuwa neno langu halimo ndani yenu maana mnataka kuniua. Yesu alikuwa anawaambia kuwa najua ninyi ni watu wa agano  na ina maana kama ni Imani walikuwa nayo maana Imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa neno la Mungu

~~Maana yake ni kuwa kuna neno walilotakiwa kuwa nalo ili waweze kutembea nalo lakini kwa wakati huo walikuwa hawana na kwa mujibu wa Yohana 4:23 Yesu alikuwa anawaambia kuwa ule msimu wa kumuabudu Mungu kama zamani umepita na sasa ni saa ya kuanza kuabudu upya yaani *katika roho na kweli*

~~Kwa sababu katika nyakati zile roho ya mwanadamu ilikuwa imekufa yaani ilikuwa haina uhai ila kwa nyakati hizi baada ya Yesu kwenda msalabani na kufufuka, roho zetu zilifufuliwa  na kuzaliwa mara ya pili na ndio maana inatakiwa tumuabudu Mungu *katika roho na kweli maana roho ziko hai sasa*

~~Yesu alisema wataniabudu katika roho na *kweli* sawa sawa na Yohana *17:17*  biblia inatumbia kuwa uwatakase kwa ile *kweli* maana neno lako ndilo *kweli*. Neno *kweli*  katika Yohana 8:32 biblia inatusmbia kuwa tutaifahamu kweli nayo kweli itatuweka huru. Kweli inapoungana na roho yako unapokuwa unamuabudu Mungu unapatana faida ndani yake.

~~Kitu gani kinaweka ufa kati ya moyo na mdomo wako, angalia Yohana 8:43 kuwa ni kwa sababu hawawezi kulisikia neno la Mungu na kama hausikii neno la Mungu ina maana unakuwa hauna Imani ndani yako maana Imani huja kwa kusikia.

~~Sasa Fikiria hawa watu wapo kanisani na Mungu anatafuta nafasi anayostahili katika maisha yao na hawampi. Unamuamini Yesu sawa, je inakuaje  uwe mwana wa Ibilisi na ukiendelea kusoma pale chini unaona wanabisha sana na Yesu ana mwisho wa siku wanaenda kuokota mawe na wanataka kumpiga Yesu kwa mawe. Alafu Yesu anapita mlango wa mchungaji na anatoka nje ya kanisa.

~~Baada ya hapo wanasema *tukuone tena* na wanaweka na Tangazo kabisa na kila cha Yesu chote wanaharibu na hao hao jumapili tena unawaona kanisani. Na Bado wanajiita wakristo.

~~Jana niliongea sentensi moja ngoja nirudie, *Mungu alisubiri Adamu awe katika hali ya mwili na Mungu aende kwa Adamu na Adamu amuabudu Mungu katika hali ya mwili lakini hakumkuta katika nafasi aliyokuwa amemuweka kwa sababu alikuwa amepoteza nafasi aliyompa, na Mungu nae alijua kuwa amepoteza nafasi ndani ya Adam*

~~Kitu kilichomuondoa Adamu katika ile nafasi na Fikra alizopotoshwa na Shetani angalia 2Wakorintho 11:3 ‘’ ```Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo```.   na Linganisha na 2Wakorintho 4:3-4 ‘’ _Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha_ *```fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu```*.

*2Wakoritho 10:3-5* ‘’ Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila *fikira ipate kumtii Kristo*

~~Lazima ujue kuwa kati ya mdomo na moyo wa mtu kunakuwa nafsi. Na ili uweze kuokoka au Mungu kuifikia roho yako ni lazima apite kwenye fikra zako. Fikra ni lango la injili la kuifikia nafsi ya mtu.

~~Roho ikitaka kutumia mdomo wako ni lazima ipate kibali kwenye fikra , na fikra ikigoma basi roho inabaki na Imani ila huku kwenye mdomo kuna kuwa na kitu kingine kabisa.Mafundisho yanaenda moja kwa moja kwenye fikra za mtu ili mtu asibaki na mapokeo  yanayomfanya apate hasara na ikifika saa ya kumuabudu Mungu awezekupata faida.  Haitoshi kuwa na Yesu mponyaji bali inatakiwa umpe Mungu nafasi na umuabudu maana kumuabudu Mungu si kitendo bali ni msimamo wa kifikra kwanza.

~~Hata mtu asiyeokoka anaweza akawa anaabudu lakini anaabudu bure, haitoshi kumwamini Yesu bila maneno yake ndani yako, maana lazima ujue ni neno gani katika biblia inatengeneza mahusiano na MUNGU Kwako.

~~Nafsi yako ikiungana na neno inatengeneza uchaji na uchaji hutengeneza kuabudu ndani yako. Na kumbuka hili kuabudu kunatangulia kwanza ndipo kunakuja kutumika. Shetani akitaka kukufunga huwa anapofusha fikra zako na anakufunga.

~~Yesu aliwafunulia akili zao ili waweze kuelewa maandiko maana akili ziko kwenye nafsi.  Na biblia inasema kama ukisikia neno la ufalme usielewane nalo huja ibilisi ili kuliondoa na akiliondoa fikra zako zinakuwa zinapofushwa.

*WAIMBAJI* Waimbaji mtanisamehe sana ila wacha niongee tu. Huduma yangu ya kwanza ilikuwa ni uimbaji na nilikuwa naimba kwaya. Japo sijajua sasa naimba sauti ya ngapi maana nilijaribu kuimba base lakini nikakuta kuwa watu wana sauti nzito kuliko ya kwangu, nikahamia kwenye vyombo lakini kuna watu walikuwa wameniwahi maana wanapiga magitaa vizuri sana. Na nikahamia kwenye kutunga nyimbo nako nikakuta kuna mabati wanapiga na ndiyo nikaanza kuyapiga.

~~ Bila wao kujua huwa hawapendi neno la Mungu na hawapendi maombi. Hata ukiwaangalia maeno mengi unakuta hawaji na biblia wala daftari  na hawapendi mafundisho na wakimaliza kuimba huwa wanadisapper kabisa na hadi baade mhubiri akiwaita tena ndio unakuta wanatokeza tena.

~~Unaimbaje sasa hauna Imani ndani yako, na hauna neno la kutosha ndio maana wayahudi walisematutaimbaje wimbo wa Bwana katika nchi ya ugeni. Kwa hiyo inatakiwa unapoimba uimbe kwa Imani  na ukisema Yesu ni Mungu awe ni Mungu kwako. Shetani anajua kuwa uimbaji huu ambao mtu anakuwa anaimba na amejawa na neno la Mungu ndani yake unabadilisha hali kabisa ya eneo na mkianza tu kuimba watu wanakaa mkao wa kuwa tayari kuwa hapa Mungu anatokeleza saa yoyote na baada ya muda mfupi wanamuona.

~~Waimbaji wanajua ni wimbo gani wa kuandaa na wimbo gani wa kuabudu. Hata Ibrahimu aliposikia ndani yake kwenda kumwabudu Mungu alienda na sadaka ya Isaka yaani sadaka ya Isaka ilikuwa ni sadaka ya kumpeleka kuabudu na ilipofika saa ya kuabudu Mungu alimpasadaka ya kuabudu maana alipewa kondoo. Sadaka ya pili ndiyo iliyofungua lango lingine. Sadaka ya Isaka ilikuwa ni ya kumpeleka mahali pa kuabudu, ili kuabudu alipewa sadaka nyingine. 

~~Unakuta saa inafika ya kumuabudu Mungu na watu ndio wanaanza kuondoka, maana sasa ndio tunaanza na Mungu ndio anakuja lakini watu ndio wanakuwa wanaondoka katikati ya saa ya kuabudu.

~~Ni muhimu sana kuomba Mungu akupe kusikia vizuri maana ni hatari sana kwako kufika mahali neno la mtumishi likawa final kwako na ukaacha kusoma biblia maana unaacha kumsikia Mungu na  kuweka neno la mtumishi mbele. Ujue kusikia baadhi ya maneno ambayo sio ya Mungu yanakufanya kuwa mtumwa na utumwa mbaya sana. 

~~Unahitaji kwenda mbele za Mungu akupe maneno yake ndani yako ili ujue namna ikupasavyo  kuabudu . Na ukifanya hivyo Mungu atashughulika na kusikia kwako ambako ndiko kutakuwa kunakutengenezea Imani ndani yako. Huwa kila siku lazima niombee kusikia kwangu maana inahitajika sana kumsikia Mungu kila wakati. Unajua ninapotaka kufundisha semina nasikia sauti ngapi? Ni nyingi sana huwa nasikia maana kuna somo la mkoa huu unataka na huku nako wasikie lakini kumbe sicho Mungu kakusudia. Hata kama nimefundisha kwa mda mrefu na miaka mingi haitakiwi nifundishe kwa mazoea na inatakiwa nifundishe kwa Imani yaani ni kitu gani Mungu anataka watu wake wasikie saa hiyo.

~~Nikitoka hapa naenda Dar es Salaam- Njombe- Mbeya – Iringa –Marekani  na kila sehemu nina somo tofauti tofuati. Na mimi ni mwanadamu kama mwanadamu mwingine nachoka kama wewe lakini kuchoka huko kusiwe execuse ya mimi kutokuomba ili MUNGU aseme na mimi kitu gani anataka kuongea.

~~Sasa chukulia nimeongea kitu potofu hapa na kama watu wengine wachanga hapa unakuta wamekufa kabisa. Kwa hiyo mimi mwenyewe kwa hii dhamana hii niliyopewa lazima niitumie vizuri kwa kusikia kitu ambacho MUNGU anataka niongee na watu wake.

~~Sasa ni hatari sana kwa mtu hujamaliza hata kusoma biblia na alafu unataka kuwa mwalimu wa neno la MUNGU. Mungu akikusemesha kutoka kwenye mistari ambayo hujasoma inakuwa ni ngumu sana kwako kumsikia MUNGU.

Endelea kutufuatilia Gospel Kitaa kwa muendeleza wa Mafundisho

www.facebook.com/felixmbwanji
Pia iko live Youtube kwa link hii https://www.youtube.com/channel/UC4p4lrpgpNd-9bHPgHJ4xWw na Ustream http://www.ustream.tv/channel/mwakasegemanaministry

Share on Google Plus

About John Maulid

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.