SOMO: MAMBO YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZITUMIKE KUFANIKISHA MAISHA YAKO (2)

SEMINA: NENO LA MUNGU
ENEO: DAR ES SALAAM
MWL: C. MWAKASEGE
▶Lengo
Kuweka maarifa ya Kiblia ndani yako yatakayokuwezesha kutumia fikra zako ili ufanikiwe ktk maisha yako
*Mith 23:7(a)*
H/W ya jana ulifanya?
✅Wapo wanaofikiri kuwa hili somo ni la wajane, sawa na huko ni kufikiri pia japo utaachwa
✅Wapo wanaofikiri kuwa ili somo ni la wastaafu sawa nao vile vile
*HATUA AMBAZO UNAHITAJI KUZIFUATA KAMA UNATAKA KUTUMIA FIKRA ZIKUSOGEZE KIMAISHA*.....[Zinaendelea...]
2⃣Tasmini kufikiri kwako ili uweze kushirikiana na MUNGU anapotaka kukusaidia kimaisha.
⚫Haifanani na hatua ya kwanza
⚫Tafsiri nyingine ni kama ifuatavyo *Mith 23:7*
_....aonavyo nafsini mwake..._
➡Biblia haisemi *aonacho* bali *aonavyo* si *afikiricho* bali *afikirivyo* si *anachotafakari* bali *anavyotafakari*
✅Kumbuka alichosema YESU kwenye *Math 13:13-14*
➡Biblia haizungumzi tu juu ya aonavyo, bali anaonavyo anachoona
➡Kinachomsaidia kuona anachoona si swala la kufikiri bali jinsi ya kufikiri
➡Ni kitu gani kinachokusukuma kufikiri na kuja na jibu ulilonalo?
*Kumbuka habari ya wale wapelelezi 12*
10:- waliona majitu
2:- waliona chakula
➡Walitazama lakini hawakuona
➡Ndivyo ilivyo wengi usoma NENO kumbe hawasomi, wengi usikiliza kumbe hawasikilizi
⚫Shida ni nini??
➡Nafsi=FIKRA zimefungwa!
*Rum 1:28*
✅Ufahamu ulioko ktk nafsi ni tofauti na ufahamu ulioko ktk roho
✅Unasema najuaje...ndiyo maana anazungumzia.habari za akili hapa...na akili haipo rohoni bali kwenye nafsi
✅Ukimkataa MUNGU kwenye fahamu zako ama kumuacha, basi utafuata akili zisizofaa, zako na za wengine!
✅Kwa sababu hyo utajikuta unafanya mambo usiyotaka kufanya
✅Kwa lugha rahisi kumwacha MUNGU huwezi tembea ktk mpango wake juu yako
✅Ukimkubali KRISTO hawezi kukuacha utembee nje ya mpango wa MUNGU
*Akili zisizofaa ni nini*
Unachotakiwa wewe kukijua/kukifuata wewe kama wewe!
Na wala si maana yake kwamba ni *akili mbaya*❌
✅Maana yake ni FIKRA ambazo kwa mtu mwingine si zake mwingine ni zake. Mfano mfanyabiashara astahili kumwona mfanyakazi ofisini anafanya kisicho sawa na vivyohivyo mfanyakazi kumtazama mfanyabiashara kuwa amepotea!
✅Ukiruhusu na kukubali MUNGU akutawalate anakupa FIKRA za kusimama alipokusudia hata kama akikuletea washauri watakushauri ktk FIKRA za MUNGU juu yako na wala hawatatumia akili mbaya
✅MUNGU anataka kutusaidia ili tuishi maisha ya kiwango cha Ki-Agano maana huko ndiko kwenye kusudi la kila mmoja!
✅Viwango vyetu vya maisha vimefungwa ktk Agano(kwa sasa twatumia Agano jipya ila tusisahau na kuliacha maana ktk lile la kale MUNGU alishaweka maagano pia)
*Hebr 8:8-10*
*Hebr 4:12-13*
➡MUNGU akitaka kukufanikisha utuma NENO ktk nafsi yako(FIKRA) ili nafsi iweze kutafsiri lile NENO kati ya roho na mwili
➡MUNGU anapotuma NENO lile NENO lina uwezo wa kutambua mawazo na makusudi ya nafsi
➡NENO ukagua aina ya FIKRA au mawazo uliyonayo ktk kuendesha maisha yako.
*Zab 117:19-20*
✅Ukimlilia MUNGU utuma NENO lake na NENO ukagua mambo haya:-
1⃣Aina ya FIKRA na akili unazotumia
2⃣Pia imsaidie maamuzi ndani yake aina gani ya akili(FIKRA) unazihitaji mahali ulipo
3⃣NENO la MUNGU linampa MUNGU nafasi ya uhalali/kibali kwako
*Isaya 55:8-11*
▶kuna pointi kama 4 hapa muhimu uzidake
*WAZO*:- MUNGU utuma wazo ndani ya mtu
*NJIA*:- Ukisha tafakari wazo ukupa njia(MIKAKATI)
*MVUA*:- Uachiliwa mvua kuzidi kunyeshea listawi na kukua hilo wazo
*NENO*:- kwa hiyo NENO ufanikiwa hakika
➡Usishtuke litakapokuja wazo tofauti na ulilonalo hyo ni ishara ya kuambiwa jipange ili utoke mahali ulipo
➡Kumbuka kama nafsi yako haitakuwa tayari kupokea hata YESU asimame mbele yako utamgomea tu, sababu ni nini mafundisho tunayopokea. *Yoh 8:31-59*
▶Ukikataa msaada wa maelekezo yake utakuwa na maisha ya kuishi jangwani tu(maisha ya mzunguko tu usijue ushike nini uache nini) na mbinguni ila jiulize Airport yako itakuwa wapi? Jangwani au Kaanani?
*TURUDI KWA MAMA MJANE TUJIFUNZE KITU*
*2Falm 4:1-7*
*MASWALI AMBAYO YANAWEZA KUKUSAIDIA KATIKA KUTATHIMINI KWAKO*
1⃣Je ninajua ni aina gani ya masaada ninaohuitaji ili niwe na maisha mazuri kuliko niliyonayo sasa?
✳Swali hili tunalipata kwa mama mjane baada ya kujieleza Elisha akamuuliza swali *nikufanyie nini*
✳Mama hakujibu lile swali hakusema anahitaji msaada gani bali alipekeka ripoti ya hali yake ya maisha aliyokuwa nayo baada ya kufa mumewe.
✳Alishindwa kujibu yawezekana kwa mambo haya:-
-FIKRA zake hazikuwa na jibu ya swali hilo
-FIKRA zake zilikuwa zimeishiwa mawazo ya kumtoa ktk shida hyo
-FIKRA zake zilikuwa zinataka kutua mzigo bila kujua atabebeshwa mzigo wa lile swali *unataka nikufanyie nini*
*MUHIMU SANA KUFAHAMU SIRI ZILIZOKO KTK MASWALI YA NAMNA HIYO*
✳ Kushindwa kujibu maswali/swali la Elisha maana yake au inaonyesha
✳Matatizo yake yalikula muda wake wa kufikiri kiasi ambacho hakubakiza muda wa kufikiria jibu
✅Muda wako ukiliwa na kukatawaliwa na matatizo huwezi fanya maamuzi, unapigwa bumbuazi huwezi pata hata wazo la kufanya ndani yako. Utabaki kukaa na hasira na huzuni
✅Usikubali mazingira yakuwekee ngome inayokwamisha/kuzuia kufikiri kwako zaidi ya mawazo uliyonayo sasa
*Mwz 26:1-14*
✳MUNGU aliisemesha FIKRA yake isitazame mazingira bali aangalie Agano
*2Kor 10:3-5*
➡Shetani upambana na kuvuruga sana FIKRA ndani ya mtu
*2Kor 11:3*
✳Unapoona mapambano ya FIKRA ndani yako usiruhusu kabisa matatizo kuyaona ni makubwa kuliko NENO ndani yako
✳Shetani uleta hila ndani ya mtu kwenye FIKRA ili kukuvuruga
*HILA MAANA YAKE NINI*
1⃣Wazo linalokuja kukuzuia uwezo wa FIKRA zako kupokea cha MUNGU na kama ulikuwa umekipokea unakikataa
2⃣Ukweli+Uongo=Usipovitenga jibu ni Uongo. Jiulize pale Edeni mti wa mema+mabaya=mabaya
✅Cheki wazo linapokuja ndani yako ROHO MTAKATIFU anasemaje? Kama si la kusudi la MUNGU utakosa amani, utapata huzuni(maana yake change your mindset fanya TOBA)
✅Uhitaji kufikiria mtu anayekuja na wazo fikiria na sikia wazo la MUNGU pekee
✅Ukikosa amani usiendelee na hilo wazo
-Cheki ndoto unazoota kama ni
✳Nyoka=kuna hila inakuja kuvuruga FIKRA zako kama kakung'ata ujue kaacha sumu na kama la jua kaacha hofu!
✳Ngome=kuna kizuizi umefungiwa ndani, ulitakiwa kutoka
✳Stendi=Kufikiri kwako kumekwama
*Unapoomba ombea sumu kuondoka na kama kuna roho ya kufuatilia utekelezaji bado ipo kemea*
*Teka kila nyara na kila FIKRA=zilizimishe kufikiri ki FLAME na KI AGANO
*HOME WORK*
✳YESU akisimama mbele yako leo akikusemesha unataka nikufanyie nini utajibu nini??
✳Ukishindwa kujibu ni wazi kufikiri kwako kumekwama!
*KWANINI MUNGU ANAULIZA MASWALI HAYA*
1⃣Kumlazimisha aliye uliza alazimishe FIKRA zake kufikiri mahali zilipokwama
2⃣Anatafuta uhalali/kibali cha kuingilia kufikiri kwako maana anaweza kuja na wazo jipya ukakataa
*..."Jesus Up"...*
*****Siku ya 2*****
Endelea kutufuatilia Gospel Kitaa kwa Muendelezo wa mafundisho
Share on Google Plus

About John Maulid

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.