SOMO: MAMBO YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZITUMIKE KUFANIKISHA MAISHA YAKO (3)

*MWALIMU*: C MWAKASEGE
*UKUMBI*: VIWANJA VYA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
*TAREHE*: 20th SEPTEMBER 2016
*SIKU YA TATU.*
LENGO LA SOMO.
_KUWEKA MAARIFA YA KIBIBLIA ILI KUPATA MAFANIKIO KWA KUTUMIA FIKRA ZAKO._
MSTARI MKUU
Mithari 23:7a
*_Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo._*
2 Wafalme 4:1-7
Hatua ya *kwanza* ilikuwa kutathmini maisha yako.
*Pili* kutathmini kufikiri kwako
Naamini Home Work ya Jana mlifanya.
Je? Unajuaje kuwa unachomuomba Mungu akufanyie ndicho mapenzi yake?
*Warumi 8:26-28*
Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.
27  Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.
Roho Mtakatifu ni Mungu ndani yako. Ni muwakilishi wa Mungu ndani yako. Muulize Roho Mtakatifu nini uombe. Roho Mtakatifu ataweka neno ndani yako. Yeye huomba sawa na mapenzi ya Mungu. Kama una neno ndani yako utajua tu. Kwenye nafsi kuna nia,hisia  nk. Roho Mtakatifu atakusaidia.
*Funzo la kwanza*
Usizuie fikra zako kushughulika na swali ambalo hujui kwanini limeulizwa. Swali la Elisha na jibu la yule mama yalikuwa tofauti kabisa. Mama hakujua kwanini swali limeulizwa na hilo likamuwekea mama ukuta ili fikra zake zisifike mbali. Ndio mana wengi wakiwa kwenye hali hii hupenda zaidi ya kuombewa kuliko kuelewa tatizo. Unapoulizwa maswali na mtumishi usimkatishe kuuliza. Huwa kuna sababu. Unapoulizwa swali ambalo Mungu tayari ana majibu nalo tatizo lipo kwenye fikra zako.
*Funzo la Pili.*
Swali la pili liliulizwa kwakuwa swali la kwanza halikufaulu kuamsha fikra za mama mjane kufikiri zaidi ya pale zilipokomea kufikiri. Mama alieleza shida zake lkn sio anataka nini! Kazi ya swali la kwanza lilikuwa kwa ajili ya kuamsha fikra za yule mama ndio mana likaulizwa la pili. Fikra zilizochoka kufikiri unazipa mzigo kufikiri kitu cha pili. Haijalishi unajaza mafuta kiasi gani kwenye gari engine ikiharibika ni kazi bure. Wazo jipya kwenye fikra zilizochoka ni kazi sana. Inawezekana Mungu anataka kuyapekeka maisha yako kiwango kingine lkn wewe unaona umechoka.
Fikra za Yesu zilichoka kabla ya kusulibiwa ndio mana wakaja malaika kumtia moyo. Mwili ukiwa umechoka akashuka mlimani. Mungu alimtia nguvu Yesu ili amalizie safari yake atakutia moyo na wewe. Ndio mana misuli ya anayepanda lift na anayepanda ngazi huwa ni tofauti. Mungu anatafuta  kinachopatikana kwako pale anaposhughulika na wewe
*Mithali 3:5*
Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
Kuna tofauti ya kutumia akili zako na kuzitegemea akili zako mwenyewe. Yani usiziache akili zako zikafanya kazi zenyewe. Akili zako hazikuumbwa zifanye kazi zenyewe. Angalia mwanadamu anapoumbwa anapuliziwa pumzi ya Mungu. Ukiwa mwanasayansi unaona oxygen lkn kiroho ni pumzi ya Mungu. Ni zaidi ya pumzi ya kawaida. Akili ziliumbwa zifanye kazi na Roho Mtakatifu na neno
*Luka 24:45*
Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.
Yesu alizifungua akili zao ili wawe mashahidi wake. Wasingeweza kufanya kazi bila Roho Mtakatifu na neno ambalo lilikuwa kwa ajili ya kuwasaidia.
*2 Timotheo 3:16-17*
Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
16  ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
Isaya 55:8-11(isome )
Akili zetu hazikuumbwa kutumia neno na roho nyingine zaidi ya ile ya Mungu.  Ili shetani aweze kutumia akili zetu aliharibu fikra kwanza. Tushindwe kutambua tubebe tu hata mabaya. Ndio mana swali la pili lilikuwa muhimu sana ili kuamsha fikra. Ndio mana unapopita kwenye magumu mengi unakuwa na maswali mengi kuliko majibu. Mengine huwa ya Roho Mtakatifu. Ndio mana hata kama anajua unachotaka bado alikupa akili zitumike. Usitumie akili bila roho wa Mungu. Ndio mana tunakwama maishani. Kuna waliookoka wamekwama na wasiookoka wanafanikiwa mbele.
*Funzo la Tatu.*
Angalia/Orodhesha vitu ulivyonavyo hata kama unaona havina thamani.
Yule mama alipoulizwa ana nini cha kwanza alisema hana kitu. Hakujua kwanini swali linaulizwa. Kwa lugha nyingine alikuwa anamwambia Elisha nilivyonavyo havina thamani ya kunitoa nilipo.
*Mathayo 14:13-21*
Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao.15  Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula.
16  Yesu akawaambia, Hawana haja kwenda zao, wapeni ninyi vyakula.
17  Wakamwambia, Hamna kitu hapa ila mikate mitano na samaki wawili.
18  Akasema, Nileteeni hapa.
19  Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano.20  Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili, vimejaa.21  Nao waliokula walikuwa wanaume wapata elfu tano, bila wanawake na watoto.
Yesu anawauliza wanafunzi wake. Kwanini mnataka watu hawa waondoke? Yesu anataka kushughulisha fikra zao. Alipowaambia kuwa wawape chakula akili yao ikaweka defence kuwa hakuna Chakula. Lkn Yesu anaona kuwa wanafunzi hawana Neno wanaangalia nje na sio ndani. Mungu ametuumba kwa namna ambayo msaada utaanzia ndani. Hata wewe orodhesha una vitu vingapi hata kama vya kurithi? Usiseme huna kitu. Hata kama ni pikipiki mbovu. Ndivyo hata kwenye kampuni yoyote wanavyofanya INVENTORY. Unahesabu vyote. Kisha angalia vipawa ulivyonavyo. Mfano unachekesha wenzio kijiweni bure lkn wenzako wanatumia huo uchekeshaji wanapata hela. Andika vyote! Usiangalie thamani
*Funzo la nne*
Unahitaji kujua kwa msaada wa Mungu kwanini unacho ulichonacho? Kwanini? Kwasababu thamani yake inategemea uhitaji wake. Yule mama alijua ana chupa ya mafuta lkn hakujua kwanini anayo. Kwahiyo hakutumia alichokuwa nacho ipasavyo?
*2 Wakorintho 9:10*
Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu;
Je,ulichonacho ni mbegu au mkate. Anayeamua ulichonacho kiwe mkate au mbegu ni Mungu. Anakupa mbegu na mkate. Nani anayeamua mbegu iwe mbegu au mkate kama mkate sio Mungu bali Fikra zako. Haijalishi amekupa mbegu au mkate anategemea ushirikiano wako. Ukitumia vibaya unavuruga utaratibu. Ndio mana usipoona vile ulivyonavyo kwenye fikra zako utapata shida. Kila alichokupa Mungu kina thamani ila fikra zako ndio huondoa thamani yake.
Yesu alipowaambia nileteeni hapa wale wanafunzi wake alikuwa anamaanisha peleka kwake kwa njia ya *Maombi.* Chochote ulichonacho au unachoona hakina thamani kwako mletee kwake. Kubariki ni kuvipa nguvu ili vifanikiwe. "To Empower and Prosper". Mfano,Isaka wa baada ya kupelekwa madhabahuni alikuwa ni tofauti na Isaka wa kabla ya kupelekwa madhabahuni. Alipopelekwa madhabahuni fikra zake ghafla zikapanuka na kuona possibilities *Oooh Hallelujah......!*.
Chochote ambacho hakiendi mpelekee Yesu kwa njia ya maombi. Mwili wako ukiuweka kwenye madhabahu ya Bwana huwa unageuzwa nia. Mungu ana mipango mikubwa kuliko gari unayotembelea. Ana mipango mikubwa kuliko chochote ulichonacho. Ndio maana ni vizuri kuweka akili zako kwa Bwana.
*Funzo la Tano*
Ukomo wa kufikiri kwako kusizuie kiwango cha utii wako katika kutekeleza wazo ulilipewa na Mungu
*2Wafalme 4:6*
Ikawa, vilipokwisha kujaa vile vyombo, akamwambia mwanawe, Niletee tena chombo. Akamwambia, Hakuna tena chombo. Mafuta yakakoma.
Mwisho wa kufikiri kwa mama mjane lilikuwa ndio mwisho wa mafuta kupatikana. Thamani ya mafuta haikuwa kwenye mafuta bali kwenye fikra zake. Vyombo alivyoleta kwa mtumishi Elisha ndio ukawa mwisho wa kupatikana kwa mafuta. Unapomuwekea Mungu mipaka unajiwekewa mipaka wewe mwenyewe. Hii ni muhimu. Mungu hukuletea Neno na Roho wake vikusaidie lkn utekelezaji wa akili (fikra zako) huwa una maana sana kwenye utekelezaji wa namna Mungu anavyokusaidia.
Fundi akiharibu kitambaa chako cha suti thamani ya Fundi ipo kwenye;
1. Kusikiliza vizuri
2. Kufikisha ukomo wa namna anavyopaswa kukitumia kitambaa.
Wengi wanaishi maisha "substandard." Wanapopata maisha ya *mtumba* "wanaridhika". Lkn Mungu ana maisha *mapya* anayotaka uwe nayo. Fikra zako ndio mwisho wako. Suleiman alipomjengea MUNGU nyumba aliijenga vizuri sana na kabla Mungu hajaingia aliridhika nayo kwanza.
Kwanini unataka Mungu aingilie maisha yako wakati ulivyojiweka mbele za Mungu ni kiholela holela tu. Haiwezekani.  Ukishinda vita kwenye fikra utashinda maisha kwenye mwili. Kiongozi yoyote ni lazima awe trained fikra zake. Uongozi sio cheo ni mtazamo wa kifikra. Pressure ikija fikra zitakuumbua kwakuwa huna utulivu wa fikra.  Ni lazima ujiweke kwenye madhabahu ya Bwana usafishwe. Mungu atakupa akili kwakuwa alikuumba yeye.
*Glory to God ....... Glory to God!*
Kama mpo Partnership ni lazima muwe na nia moja. Ndio mana ni lazima kwenda mbele za Bwana kuomba ili muwaze na kunia mamoja. Kama mwenzako anasema 3 na wewe unasema 5 lazima mtagombana. Mnapaswa kunia mamoja. Muombe Mungu upate partner ambaye mtania mamoja...
Mungu alipotuumba alitaka tufike mbali sana. Dhambi ikaharibu. Pata picha pamoja na dhambi zetu bado tunarusha madege makubwa angani je kusingekuwa na dhambi tungefanya nini? Akili ni fursa.  Unaona pale mwingine asipoona. Kuna fikra nyingine hazioni kesho. Zipeleke fikra kwenye madhabahu ya Bwana.  Naye atafanya.
Tuombe....
Endelea kutufuatilia Gospel Kitaa kwa Muendelezo wa Mafundisho
Share on Google Plus

About John Maulid

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.