SOMO: MAMBO YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZITUMIKE KUFANIKISHA MAISHA YAKO(4)

SEMINA: NENO LA MUNGU
ENEO: DAR ES SALAAM
MWL: C. MWAKASEGE
SIKU: 4

▶Lengo
Kuweka maarifa ya Kiblia ndani yako yatakayokuwezesha kutumia FIKRA zako ili ufanikiwe ktk maisha yako

*Mith 23:7(a)*

*Summary*
➡Tuliangalia maana nzima ya FIKRA
➡Tuliangalia hatua ya kwanza
➡Tukafahamu na ya pili
➡Tukapena na H/W, jitahidi sana kuomba mara kwa mara juu ya hizi H/W hasa ile ya jana maana ni mtaji kwako na usifanyie utani
➡Tukaangalia jana na mafunzo kadhaa kama 5 hivi

*LEO*
✅Tunaendelea na ule mstari wa *7*
*2Falm 4:1-7*
✅kipengelea cha muhimu au nataka uone hapa ni pale Biblia inaposema....... *enenda ukayauze mafuta haya*.........

✅Ningekuwepo kipindi hiki ROHO MTAKATIFU anamvuvia upako mwandishi wa kitabu hiki ningemwambia aongeze kidogo hii habari ya mama mjane kujua *jinsi alivyouza mafuta haya* maana Biblia haikuendelea kusema

✅Maana hakuwa mfanyabiashara, alikuwa mgeni sokoni, ni mara yake ya kwanza kuuza

✅Je somo la kuuza alipata wapi? Je aliuza? Kwa shs ngapi?

✅Maana waweza kuwa na vitu na usiuze pia maana si kitu chepesi atii, wafanyabiashara wanaelewa. Jiulize Mama mjane hakuwa na hata na lebo kwenye mafuta yake, packing ilikuwa na kumbuka vyombo vilikuwa vya kuazima maana yake mafuta yako kwenye vyombo tofauti tofauti, alifungajefungaje?

*JAMBO LA MSINGI*
✅Ni kuwa Elisha alitumika kumtengenezea kuandaa FIKRA zake zaidi kwa habari ya soko.

*FUNZO LA 6⃣*
Jifunze na jizoeze kulitafuta na kuliona na kuliingia soko kiroho kwanza kwa njia ya FIKRA zako kabla ujaliona soko hilo iwe kimwili ama kiuchumi

➡Utekelezaji wa mstari wa 7 unategemea sana utekelezaji wa ile mistari.kuanzia wa 3-6

➡mistari ya 3-6 Alitekeleza kwa kiwango gani maagizo aliyopewa

➡Maana 3-6 maagizo haya yalikuwa ya kujenga FIKRA zake ziweze kuona thamani ya chupa ya mafuta kwa jicho la FIKRA zake.

➡Ndani ya FIKRA zake lazima uhitajiwa (soko) wa chupa ya mafuta

➡MUNGU alimtengenezea ya kuwa kama ulichonacho hakina thamani kwenye FIKRA zako hakiwezi kuwa na thamani kwenye soko

*SABABU HIYO*
✅FIKRA lazima zione thamani ya kitu(uhitajiwa wake) ndiyo kitakuwa na thamani sokoni

✅Wengi wamekufa na kuviacha vitu vingi sana sababu ya kushindwa kitambua uthamani wake hata hivi leo kupotea bila faida

✅Soko linaonekana kwanza kwenye FIKRA kabla ya nje

*Wakati mama mjane anapewa maelekezo aliambiwa*

*I).* Nenda, halafu koma(,)
Maana yake fikra zake ziwe na utayari wa kutafuta soko. Yalikuwa maamuzi ya ndani

*II).* Nenda ukatake vyombo kwa jirani zako wote
✅Alikuwa anaambiwa panua wigo wa vyombo vitupu
✅MUNGU alitaka aone uhusiano wa chupa ya mafuta na FIKRA zake pamoja na soko la mafuta
✅Kati ya chupa ya mafuta na soko la mafuta katikati yake kuna FIKRA
✅FIKRA zikigoma soko la mafuta limegoma

✅Kwa hiyo uhusiano kati ya chupa ya mafuta, FIKRA na soko ni wa *KIROHO KWANZA.*

✅Kwa lugha nyepesi Soko ni mkutaniko wa wauzaji na wanunuzi

✅Mtu anayeuza anategemea soko kuuza, soko kumkutanisha na mnunuzi, soko kumpa bei, soko kumwandalia auze lini kwa kiasi gani

✅Anayenunua naye anategemea soko limkutanishe na bidhaa anayoitahi, soko limpe bei, limkutanishe na muuzaji, limwekee utaratibu wa kununua

*SOKO LINAANDALIWA NA NANI*
➡Wauzaji/muuzaji
➡Mununuzi
➡Wote kwa pamoja
➡Yule ambaye upata faida kwa Mnunuzi na Muuzaji kukutana (Serikali)

✳Soko linatakiwa kutawalina na nani? Na linatawaliwa na nani?

✅Soko uandaliwa kwenye FIKRA (msukumo wa kuhusisha ulichonacho na soko)

✅Soko ni la KIROHO KWANZA
*Isaya 24:1-2*
✅Adhabu ya kiroho ilienda kugusa maeneo tofautitofauti imegusa mpaka soko
-Muuzaji na Mnunuzi wanafanana
-Mkopaji na Mkopeshaji wanafanana

*Eze 7:12*
➡Muuzaji na Mnunuzi kuna adhabu mjini

*Neh 13:15-22*
➡Viongozi kutumia misingi yao ya imani kubana aina fulani ya soko
➡Kiongozi alifunga milango kuzuia biashara sababu ya misimamo yake ya kiimani

✅Kwa hiyo nguvu ya hilo soko halipo ktk vitu vinavyouzwa bali ktk ulimwengu wa roho

✅Imani kuanza kuingia kidogo kidogo kwenye uchumi kuwa na uhakika utegemea ni imani ipi na ina ingiza nini ndo maana soko uanzia rohoni kwanza.

*Uf 13:1-7*
➡Roho ya mpinga kristo ukimbilia kushambulia kwenye eneo la soko

➡Ndo maana watu.wenye haki/walokole wengi wanapambana hapa shetani anajaribu kuwazuia kwenye eneo hili ili wasifanikiwe na wengine hawajui kwanini kila biashara kwako inagoma au yeye auzi na wale wenzake wa mataifa wanauza kweli. Shida ni kutokujua na kutofundishwa kuona soko rohoni kwanza.

*SWALI*
Wangapi hawana Akaunti Benki? Ila wengi hawajui kwanini hawataki kugungua akaunti benki. Sasa sikwambii huna pesa au napigia debe Benki noo
Mfano Mfanyakazi unapokea mshahara ukatoa sadaka zako na kilichobaki kikarudi benki uwe na uhakika kimerudi na ROHO wa MUNGU kwenye mzunguko wa fedha yako

➡Pesa haina dini bali ina Roho.

*Uf 18:1-3,9-13*
➡Hakuna mtu anayenunua bidhaa yao tena si kwamba soko halipo

➡Si kila mfanyabiashara utafuta msaada sehemu nzuri

➡Kuna anaye amua kipi kinunuliwe na kipi kisinunuliwe usipoweza kujua hapo na kutengua hapo utateseka

*NANI ANATAWALA SOKO LA AJIRA?*
➡Ulimwengu wa roho utawala soko hili

Jifunze kwa kina Daniel walikuwa bora mara 10 ya wale waliomzunguka mfalme! Maana mfalme hakuwa na kauli ya mwisho na sababu kina Daniel walikuwa bora zaidi kilimbana mfalme kuwaondoa wale wachaw na nafasi hizo kupewa kina Daniel.

*Uf 5:9-10*
*....ukamnunulia MUNGU.....*
✅DAMU YA YESU ina ruksa kuingia sokoni sababu kuna kitu kilichokuwa kinauzwa kimewekwa bei ya juu ili kisinunuliwe

✅YESU alijua thamani ya DAMU yake na alitununua kwa cash.

✅Kwa kutumia DAMU ya YESU waweza ingia kama mfalme sokoni
✅Usijizuie omba kila ufikapo dukani kwako anza kwa maombi
✅mahali ambapo soko halina haki kuna dhuruma na mambo si ya KIFALME achilia DAMU ya YESU isemeshe ardhi ya mahali hapo

✳Usiende kwenye soko bila DAMU ya YESU
✳Hakikisha FIKRA zako zimepata kibali cha NENO la MUNGU na ROHO MTAKATIFU
✳Ombea kibali juu ya Biashara yako
✳Hakika ROHO MTAKATIFU anajua anayehitaji bidhaa unazouza

*Math 6:33*
➡Hakikisha mfumo wa UFALME wa MUNGU umekaa juu ya soko

➡Mfumo.unatengenezwa, tafuta haki mfumo wa Kiblia wa Biashara (soko) uliopotea

➡Maana bila mfumo hakuna uwajibikaji. Mfumo.wahitajika kila mahali iwe kanisani mpaka kwenye familia..

*HOME WORK*
✳Unaona soko kwenye FIKRA zako kwa kiwango kipi?
(Fursa zako za kuuza na kununua na kuuza tena)

✳Cheki mahali unapofanyia Biashara kama kuna umiliki wa KIROHO/KIFALME

*MAOMBI*

*..."Jesus Up"...*

*****SIKU YA NNE*****
Endelea kutufuatilia Gospel Kitaa kwa muendelezo wa Mafundisho

Share on Google Plus

About John Maulid

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.