SOMO: MASHIMO YA KICHAWI (3) - ASKOFU GWAJIMATumejifunza kwamba shetani amejenga ufalme wake Baharini, angani na ardhini/kwenye nchi ambapo kuna mashimo makuba ya makazi yake.


Mungu alimpa mwanadamu huo uwezo wa kumiliki lakini shetani aliutwaa kutoka kwa mwanadamu baada ya kumdanganya.

Mwnzo 1: 26 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.”

Mashimo haya makubwa yapo angani, ardhini na baharini
Luka 8:30 “Yesu akamwuliza, Jina lako nani? Akasema, Jina langu ni Jeshi; kwa sababu pepo wengi wamemwingia. Wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni.”

Yesu alipovuka ngambo alikutana na mtu mwenye mapepo mengi ndani yake kiasi kwamba alikuwa akijikatakata na kuwazuia watu wa mji wasipite njia ile. Bwana Yesu alipofiika pale mapepo yalimtambua kwamba yeye ni mwana wa Mungu ndio maana yakamwomba asiwarudishe kwenye shimo la baharini yakamwomba yawaingie nguruwe waliokua karibu.

Ufunuo wa Yohana 10:5 “Na yule malaika niliyemwona, akisimama juu ya bahari na juu ya nchi, akainua mkono wake wa kuume kuelekea mbinguni”

Tunaona Malaika huyu amezuia shimo la angani, ardhini na baharini ili Utukufu wa Mungu udhihirike.

Yeremia 7:18 “Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha mimi.”

Yeremia 44:19 “Nasi tulipomfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, je! Tulimfanyizia mikate, ili kumwabudu, na kummiminia mamiminiko, waume zetu wasipokuwapo?”

Daniel10:12 Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako. Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.”

Kila shimo lina mfalme na malika wake, kama unaumwa miguu au uzazi fahamu ipo imechukuliwa kabisa shimoni inatumika kujenga ufalme wa giza, cha msingi unatakiwa ubaini ni eneo gani linakusumbua uamue kupigana kwa Damu na jina la Yesu kriso.

Waefeso 6:12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”

Yeremia 51:20 “Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme; na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunja-vunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake; na kwa wewe nitawavunja-vunja mwanamume na mwanamke; na kwa wewe nitawavunja-vunja mzee na mtoto; na kwa wewe nitawavunja-vunja kijana mwanamume na kijana mwanamke; na kwa wewe nitamvunja-vunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe nitamvunja-vunja mkulima na jozi yake ya ng'ombe; na kwa wewe nitawavunja-vunja maliwali na maakida.”

Ukishafahamu hayo unasimama Katika Jina la Yesu namwendea aliyechukua miguu yangu namfuata naichukua kwa jina la Yesu, narudisha akili yangu kwa damu ya Yesu, unarudisha ndoa, macho, mikono, uso wa upendeleo, nyota, moyo, tumbo la uzazi, kwa jina la Yesu.

Ukiwa unaomba hivyo kwa mamlaka hutaona chochote lakini kishapishindana kwa muda utaanza kuona vitu vyotev inarudi na unaanza kuona umepona kama ulikua unaumwa ukienda hospitali unapona mara moja kwasababu umeshaharibu chanzo cha tatizo lakini usiposhindana na chanzo cha tatizo utazunguka kila sehemu bila kupata ufumbuzi, kama ulikua unakosa kazi kila ukiomba utashangaa unaanza kuitwa uanze kazi kwasababu umerudisha nyota yako iliyoibiwa kwa jina la Yesu, umerudisha kinywa cha kuongea vizuri, kama ulikua hupendwi kazini na wenzako utashangaa unaheshimika na kusalimiwa, kama kulikua hakuna mtu anayekuambia anakupenda utashangaa unaambiwa umependeza kwasababu umerudisha asili yako ya kibali na mvuto kwa jina la Yesu.

Mkuu wa anga anamiliki maeneo hayo sababu ni sehemu ambayo mwanadamu amepewa na Mungu tangu asili ili amiliki hivyo kwasababu anataka kuabudiwa ameyamiliki na hazina zake ili mwanadamu akitaka kufanikiwa amwendee yeye kwanza ili atumie binadamu haohao wamtumikie kuujenga ufalme wake aje aimilki dunia kama mpinga kristo.

Unapokuwa umeguswa kuomba jambo kwa wakati fulani unatakiwa uombe mpaka usikie moyoni pametulia ndipo uache sababu “HATUOMBI ILI TUJIBIWE BALI TUNAOMBA MPAKA TUJIBIWE".

Kama ni Mungu tunaye, kama ni Baba tunaye mwenye majigambo ya kutisha na ana majina mengi mfano anajina lake anajiita NIKO AMBAYE NIKO, kama kuna mambo ya kutafuta basi tafuta lakini sio Mungu. Hiyo bahari unayoiona ni yeye aliiumba, hii dunia unayoiona na jua na mwezi na sayari zote na anga la sayari na nyote vyote hivyo aliyeviumba ni Mungu tunayetangaza habari zake ni Mungu tunaye mwabudu ni Mungu mwenye kutisha ni Mungu mwenye wivu kama anavyosema mwenyewe.

Mwanzo 1:1 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.”

Kumbukumbu la Torati 32:39 “Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye, Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi; Naua Mimi, nahuisha Mimi, Nimejeruhi, tena naponya; Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu “

Kutoka 20:5 “Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao”

KUNA MAMBO 10 YA KUYAJUA AMBAYO KUZIMU INAYO

1. MAKOMEO

Ayubu 17:16 “Litashuka kwenye makomeo ya kuzimu, Itakapokuwapo raha mavumbini”

Ukiibiwa furaha yako, akili yako, familia yako, ndoa yako haziwekwi sehemu nyingine yeyote inawekwa chini/ kuzimu inawekwa kule na haitoki hivihivi kwa kulalamika au kulia au sala za kawaida dawa ni kuvunja makomeo yalioshikilia ndoa yako mpaka imekua hivyo, vunja makomeo yalioshikilia akili yako na tabia mbaya uliyo nayo kwa jina la Yesu.

2. MILANGO
Ayubu 38:17 Je! Umefunuliwa malango ya mauti, Au umeyaona malango ya kuzimu?

Isaya 38:10 Nalisema, Katika usitawi wa siku zangu nitakwenda kuingia malango ya kuzimu; Nimenyimwa mabaki ya miaka yangu.
Mahali penye komeo lazima kuna mlango. Penye mlango ni mhali watu wanaingia na kutoka.

Wakala wa shetani wakichukua akili,macho, nyota au tumbo la uzazi wanatumia na kuzuia kwenye milango hiyo na kuna walinzi wazuiao.

Mathayo 16:18 “Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.”

Milango ya kuzimu haitatushinda sanabu tumepewa uwezo wa kuwanyanganya wakala wa kuzimu na kuwapiga kwa jina la Yesu. Unapoomba unasema katika jina la Yesu nashambulia malango ya kuzimu kwa damu ya Yesu achia biashara yangu kwa jina la Yesu…. achia halafu unapiga komeo zake sababu kila mlango una komeo lake (milango na makomeo hayo ni mpepo) ukiomba kwa mamlaka utashangaa akili yako inarudi, macho yako yanarudi, unaanza kuona tena

3. KAMBA.

2 Samweli 22:6 “Kamba za kuzimu zilinizunguka; Mitego ya mauti ikanikabili.”

Zaburi 18:5 “Kamba za kuzimu zilinizunguka, Mitego ya mauti ikanikabili.”

Tumeona kuna mlango ya kuzimu ambako ndiko shimoni, pia kuna makomeo halafu humo humo ndani ya shimo kuna kamba zinazofunga. Tunaona kumbe biashara inaweza kuchukuliwa ikaingizwa shimoni kupitia mlangoni halafu ikafungwa kwa kamba mlemle ndani ya shimo. Sasa unapoomba unazungumza na kamba zenyewe kwa jina la Yesu sababu zinasikia ni roho kamili zenye uwezo wa kusikia.

Ukiri.
"Ewe kamba nakuamuru achia afya yangu kwa damu ya Yesu, mimi ni mali ya Yesu”

Zaburi 30:3 “Umeniinua nafsi yangu, Ee Bwana, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao shimoni.”

Ukielewa hapo utashanga vita yako inkuw rahisi unapiga shimo la angani, shimo la baharini na shimo la nchi halafu unapiga mashimo madogodogo kwenye dari, miti mikubwa, mashambani, mashimoni, maporini, kwenye makabati, nyuma na mlango n.k haya ni mashimo madogomadogo ambayo wachawi huyatumia yapo kabisa.

Ukielewa maarifa haya ukiwa unaomba unajua upige wapi unakua una maarifa kamili unapiga milango, kofuli za shimoni, kamba shimoni unakuwa unauhakika wa ushindi asilimia miamoja kama mwanajeshi wa Bwana kwa jina la Yesu.

4. MAKAO

Zaburi 49:14 Kama kondoo wamewekwa kwenda kuzimu, Na mauti itawachunga; Watu wanyofu watawamiliki asubuhi; Umbo lao litachakaa, kao lao ni kuzimu. Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu, Atanitoa mkononi mwa kuzimu, maana atanikaribisha.”

Mfano wa makao ya kuzimu ni pale unapoweza kumkuta mtu ni mgonjwa, au maskini, au hajasoma au ameshindwa kufanya biashara amekata tama na nafsini mwake amakubaliana na hali aliyo nayo anasema nimeshazoea bora mkono kinywani n.k ukiona hivyo fahamu mtu huyo yupo kwenye mkao ya shimoni amelazwa kule japo huku duiani anaonekana kimwili yupo lakini ndani amelazwa ameibiwa ama nyota ama akili yale na moyo wake unatumika pahala. “Kuzimu wanatoka Jehanamu ndio hawatoki”
Yesu alikuja duniani kwa kazi ya kutukomboa na kuushinda ulimwengu, alitununua kwa damu yake akautoa uhai msalabani na kwenda mpaka kuzimu kuwahubiria roho zilizolizokuwa kule na kuzitoa huko kwenda mbinguni (kabla Yesu hajaja watu walikuwa wakifa hawaendi mbinguni walikua wanaenda kuzimu lakini eneo la watakatifu wakitenganishwa na shimo kubwa katikati ili wasivuke kwenda upande mwingine).

Ufunuo wa Yohana 1:18 “na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu”

Hivyo kuzimu wanatoka. Bwana Yesu alimwendea shetani mpaka kuzimu akamnyanganya funguo za mauti na kuzimu kasha akamponda kichwa shetani ili andiko litimie.

Mwanzo 3:15 “nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.”

kwamaana shetani alimponda Yesu kisigino pale alipokuwa anateswa kabla hajaitoa roho yake msalabani Ndiomaana lipofufuka kwa wafu alisema mamlaka yote mbinguni na duniana nimepewa

Mathayo 28:18 “Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”

Kuzimu/shimoni unaweza kwenda ukiwa hai kabisa sababu wapo watu wanokwenda huko kutafuta umaarufu na utajiri.

Mathayo 4:8 “Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia. Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake”

Kuna watu wantembea leo dunini lakini ni vivuli hawa ndio wanaitwa misukule wameibiwa na kutekwa kuzimu. Huu ni ujumbe ambao umejificha kwenye mataifa mengi Duniani ambao ukiuhubiri mahali watu wengi wanatoa macho sababu hawajui wamepofushwa kwamba kila kinachoendelea ni mapenzi ya Mungu, watu wamefungwa kwa imani za misingi ya kibinadamu kwenye dini na kuabudu wasicho kijua lakini huu ndio wakati wa kuwarudisha wote walioibiwa kwa mamlaka ya Yesu, hii ndio saa ya kazi ya Bwana kutawala dunia kwa nguvu na udhihirisho wake kwa jina la Yesu.

Luka 16:19 “Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu. Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.”

Huko duniani wako Musa na manabii maana yake ni “Wachungaji na Neno la Mungu”. Mungu alikataa ombi la yule mtu sababu alijua watu ni wagumu kuamini hata kama mtu akitoka kuzimu akiwaambia alikua kuzimu hawawezi kumwamini sababu wanasema ni hadithi za kutungwa kwasababu ya kupata umaarufu au mambo flani flani. Maombi ya Yule Tajiri hayakujibiwa kwa wakati ule lakini nyakati hizi maombi yake yamejibiwa Mungu ameamua kudhihirisha kwa kuwarudisha watu wake walionewa kutoka kifungoni kwenye mashimo.

Yohna 5: 24 “Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani. Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai.”

Saa inakuja na sasa ipo maana yake ni siku za mwisho ambazo ni leo hii.

Zaburi 55: 15 “Mauti na iwapate kwa ghafula, Na washuke kuzimu wangali hai, Maana uovu u makaoni mwao na katikati yao.”

5. MKONO

Zaburi 89: 48 :Ni mwanamume gani atakayeishi asione mauti, Atakayejiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu?:

Shimoni au Kuzimu tumeona kuna makomeo, kuna milango, kuna kamba, kuna makao, pia kuna mikono ambayo imeshikilia watu wasirudi duniani. Mikono hii ndiyo inazuia biashara, inazuia kazi kama mtu ameenda kuomba kazi, inazuia fedha sababu mtu ameibiwa mikono ya kutafuta fedha unakuta mikono inatumika kule kuzimu huke yeye akihangaika kupata fedha bila mafanikio.

Sasa unapokuwa unaomba Omba kwa maarifa jifunze kuukata mkono wa kuzimu kwatumia maandiko unasema katika jina la Yesu natumia upanga wa Roho (unakua tayari umeshautwaa kwenye ulimwengu wa roho) mfano Imeandikwa

Waefeso 6:17 “Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu"

Unasema imeandikwa “Mimi ni rungu la Bwana na silaha za Bwana za vita…..” hapo unakua unajitambulisha kama silaha ukitumia silaha ya upanga kasha unaanza na makomeo ya kuzimu unayalishambulia kwa Damu ya Yesu unafuata malango, unaharibu na kamba zake unazikata kasha unaharibo mikono iliyo kushikilia kasha unarudisha vyote vilivyomezwa na kuzimu kwa mamlaka ya jina la Yesu.

Watumishi wengi wa Mungu hawataki kutoa maarifa kwa watu wanataka wao ndio wawe wanatatua matatizo ya watu ili waonekane "superial" zaidi kitu ambacho sio kizuri kwasababu ili kanisa liwe na nguvu inatakiwa kila mtu ajue kupigana vita vya rohoni na awe na maarifa japokua ni sawa kuombewa lakini isiishie hapo ikiwa kila mtu anashindana kwa maarifa kwa jina la Yesu, shetani hatapata nafasi juu ya maisha ya watu na sababu kama na kila akisimama mahali pake akashindana rohoni kwa maarifa kama haya kama ni taifa linabadilika na kustawi sababu linakua limekombolewa rohoni na kanisa linakua na nguvu kubwa kwa damu ya Yesu krito.

Ukiamua kufunga hata siku mbili unasema unywe maji tu ukanaa unajifungia huongei na mtu kurudisha vyote vilivyoibiwa na kuzimu unaanza kujitakasa kwa maandiko ya msamaha wa dhambi kasha unaomba hivyo kwa juhudi ukianza taratibu ili usichoke haraka utashangaa baada ya maombi utaanza kuwa unaota umeshika upanga na utawaona wanakujia kwenye ndoto wakikuuliza mbona unawanyanganya ukiona vyovyo ujue tayari umewashinda na umesharudisha vyote kwa jina la Yesu.

Ukimwina mtu anashida ujue ni mkono wa kuzimu

6. SHIDA

Zaburi 116:3 :Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni;”

"Shida za kuzimu zikikupata" Ukiwa na shida na taabu iharibu na ukiivunja inaharibika maana ni mapepo yenye kuleta taabu ambayo hayatoki kwa kuombewa tu mara moja sababu yatarudi tarudi, unatakiwa ujifunze kupigana kwa jina la Yesu.

7. KITANDA

Zaburi 139:8 :Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.”

Kama kuzimu kuna kitanda basi ndio maana watu wameibiwa wakafungwa huko kwa kamba za kuzimu na milango ya huko imewazuia wasitoke, lakini sauti imeshapatikana ambayo kwa mamlaka yake wanarudi wote sauti hiyo ni Yesu kristo ametupa mamlaka juu ya kuzimu na mauti na sisi tunaweza kurudisha vyote na kuwatoa waliobiwa kwa jina la Yesu. Amen
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.