TAMASHA LA UWEPONI MWAKO SEPT 11 MITO YA BARAKA DSM


Jumapili ya tarehe 11 mwezi huu wa Septemba, kwa mara nyingine The Joshua Generation wameandaa Tamasha kubwa sana ambalo hili litafanyika mchana kuanzia saa nane kamili na kuendelea.. watakupa nafasi pia kuzifahamu nyimbo zao katika album yao ya kwanza. kama vile Mbele yangu, Hossana, Hakuna, U mwaminifu, pamoja na nyingine nyingi.

Lakini huenda unawasikia tu na huwatambui vema.
THE JOSHUA GENERATION  ni jina la kinabii (prophetic name) hiki ni kikundi cha uimbaji ambacho kilianza rasmi mnamo mwanzoni mwa mwaka 2014, kikiwa na idadi ya watu 18.

Malengo waliyokuwa nayo na kuwapelekea kuanzisha upya kikundi hiki cha uimbaji baada ya hapo awali kutofanya vizuri miaka ya 2012..kubwa zaidi ni kumsifu na kumwimbia Mungu katika roho na kweli,lakini pia kufanya huduma ya kuwaleta watu kwa Yesu.

The Joshua Generation tangu ilipoanzishwa mnamo mwaka 2014 mpaka sasa imefanya matamasha makubwa mawili, 2014 tamasha la utambulisho wa kikundi, na pia mwaka 2015 likafanyika tamasha jingine lililopewa jina la the night of redemption( usiku wa ukombozi).

Mpaka sasa kikundi hiki kina zaidi ya watu 29 kikiwa na wawakilishi pia mataifa mbalimbali kama vile marekani,China na India pia. Na kikundi hiki kiko chini ya ulezi wa Askofu Dr Bruno .R. Mwakibolwa Katika kanisa la E.A.G(T) Mito ya Baraka huku pia kanisa hilo likiwa na Neema ya kuwaibua waimbaji wengi amboa wamefamika na n nje ya Tanzania (UTUKUFU KWA MUNGU)

Tamasha la Jumapili hii litakuwa ni kusifu na kumwabudu Mungu wetu.. Na limepewa jina UWEPONI MWAKO.

Kanisa la EAG(T) Mito ya Baraka lipo Kariakoo Jangwani karibu na jengo la timu ya mpira wa miguu ya Yanga.
Share on Google Plus

About Silas Mbise

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.