USHAURI WANGU KWA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI

John Maulid,
Staff Reporter.

Waimbaji hasa waliotangulia kusikika ama kujulikana na jamii napenda wawe na ushirikiano mzuri na waimbaji hawa wanaochipukia maana huwa wanalalamika Sana kuwa hawapati ushirikiano mzuri hasa pale anapomfata mwimbaji aliye juu kumuomba ushauri.

Au unakuta kama mwimbaji wa kike anaechipukia akimfuata mwimbaji wa kiume aliye juu kimziki kuna maneno anaambiwa yule binti hadi anavunjika moyo kabisa,  waimbaji tuenende kama atakavyo
BWANA Mungu.

Sote tuitangaze injili ya BWANA wetu Yesu Kristo. 

Nimependa sasa hivi kuna vipaji vingi vinachipukia na wanafanya vizuri katika soko na katika vyombo vya habari. Nimependa uimbaji wao kama huyu Dada Oliver Wema; ukimsikiliza uimbaji wake kama Rose Mhando, ndiyo sauti yake na yeye aliyopewa na Mungu. 

Pia unakuta ni upenzi unajua ukimpenda mtu basi utataka ufanye kama yule mtu unayempenda ndiyo maana huwezi kuwatofautisha

Muimbaji mwingine nimeanza kusikia nyimbo zake hivi karibuni ni Debora Lusinde, huyu dada nae uimbaji wake ukiusikia ni kama Martha Mwaipaja. Ukiiona video ndiyo utatambua kuwa siyo Martha. Hivyo napenda kuwasisitiza kwamba kwakuwa wote wanamtukuza Mungu mmoja kwa njia ya uimbaji naombeni tuwe na ushirikiano watu wa Mungu.Share on Google Plus

About John Maulid

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.