BABA NA U NDIO CHAGUO LA GK NI KIWANGO 'LIVE' KUTOKA LAGOS NIGERIA

Paul Chisom Udo
Chaguo la GK hii leo tupo jijini Lagos nchini Nigeria ambako tunakutana na kaka matata kwenye huduma ya muziki wa injili anayefahamika kwa jina la Paul Chisom Udo a.k.a PC. Wimbo tuliokuchagulia ni moja kati ya nyimbo maarufu kutungwa na kijana huyu ambaye alifunga ndoa hivi karibuni, hapa akiwa amerishirikisha kundi maarufu la injili la nchini humo liitwalo Lagos Community Gospel Choir (LCGC).

Wimbo huu 'Baba Na U' wimbo ambao umebeba maana kubwa ya kumtafakari Mungu kwamba bila yeye tusingeweza lolote, maana yupo pamoja nasi kila hatua katika maisha yetu.  Nina uhakika kwamba utakubariki ingawa itabidi ikuchukue muda kuelewa kiingereza cha Kinigeria ambacho ndicho kilichotumika katika wimbo huu waliorekodi live katika moja ya tukio jijini Lagos Nigeria.

Pia unaweza kumuona mwanakaka huyu ambaye tayari alitembelea nchini Tanzania mwaka juzi na baadhi wa waimbaji wenzake kutoka Nigeria katika mwaliko wa moja ya kanisa lenye watumishi kutoka nchini humo, akiwa pia na kwaya ya LCGC katika wimbo maarufu nchini humo uitwao 'Chukwu Ebuka' ulioimbwa kwa lugha ya kabila maarufu na kubwa nchini Nigeria la Igbo. Barikiwa uwe na jumapili njema

Lagos Community Gospel Choir (LCGC)Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.