CHAGUO LA GK TUPO NA NDUGU ZAO JOYOUS CELEBRATIONYawezekana kuna baadhi ya watu wanalijua kundi la Spirit of Praise pamoja na Worship House kuwa ndio wanaoifuatia Joyous kwa karibu huku wakiwa wameisahau ama hawaijui kwaya nyingine inayojinyakulia umaarufu nchini Afrika ya kusini ya Tshwane Gospel Choir ambao chaguo la GK kwa leo linatoka kwao.

Kwaya hii haina muda mrefu sana kulinganisha na Joyous au Spirit of Praise lakini tayari imejulikana vyema ikiwa sambamba na kurekodi na waimbaji maarufu akiwemo mwanamama Dkt Rebecca Malope, Loyiso Bala na James Fortune. Wapenzi wa Joyous wanaofahamika kama tot waliipachika kwaya hii jina la Joyous fake ama bandia kutokana na jinsi wanavyoiga kundi hilo.

Wimbo tuliokuchagulia kutoka kwao unaitwa 'Mehlo a Bona Ke Metsu' unaopatikana katika DVD yao ya Modimo ya Mehlolo waliyoitoa mwaka 2014 ukiwa umeimbwa na mwanakaka Godfrey Mahlangu. Kwasasa wana DVD mpya waliyoitoa hivi karibuni, lakini pia wanatarajia kuwa katika jukwaa moja na gwiji wa muziki wa injili duniani pastor Donnie McClurkin mwezi huu pamoja na waimbaji wengine nyota wa Afrika ya kusini.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.