MAZISHI YA WINNIE JACKSON BENTY TAREHE 11 NJIRO, ARUSHA

Marehemu Winnie Jackson Benty ©FB/Jackson Benty
Heshima za mwisho kuuaga mwili wa marehemu Winnie Jackson Benty ama Mrs Benty (mke wa muimbaji nyimbo za injili na kiongozi wa sifa Kanisa la Ufufuo na Uzima Arusha, Jackson Benty) zitafanyika Jumanne tarehe 11, maeneo ya Njiro. Msiba ukiwa umewekwa nyumbani kwa marehemu, Kwa Mrombo karibu na bomba la maji ya jeshi.


Taarifa za awali ambazo Gospel Kitaa imezipata zinaeleza kwamba marehemu ambaye alikutawa na umauti Burka, Jijini Arusha - kutokana na ajali iliyohusisha basi la kampuni ya Mtei Express na pikipiki aliyokuwa amepanda.

Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Mount Meru, ambapo ibada ya mazishi itaanza saa  tano asubuhi hadi saa saba mchana kisha kufuatiwa na msafara wa kwenda makaburini, Njiro.

Winnie ameacha mgane na watoto wawili, mkubwa akiwa na umri wa miaka mitano.

Jackson na Winnie pamoja na mtoto wao, Joshua. ©RumaAfrica
BWANA ametoa na BWANA ametwaa, Jina la BWANA lihimidiwe.

Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.