MY PRAISE CONCERT NI LEO KILIMANJARO MASAA MACHACHE YAJAYO USIKOSE GK TUTAKUWEPOIlikuwa tunahesabu siku lakini sasa tunahesabu masaa tu ili kile kilichokuwa kinasubiriwa kwa hamu na shauku kwa wakazi wa kilimanjaro kufanyika yaani MY PRAISE CONCERT inayoandaliwa na kikundi kinachofanya vyema sana kanda ya kaskazini kilichosheheni vijana THE HEAVENLY MELODIES.

Mazoezi ya mwisho mwisho yakiwa yanaendelea kufanyika na mambo mengine kuwekwa sawa. Taarifa ambazo hazijabadilika mpaka muda huu ni kwamba ibada hii kubwa isubiriwayo na maelfu ya watu jijini Kilimanjaro litasindikwa na Wz Abeidnego and Worshipers band watakuwepo kuhudumu na kushusha uwepo wa Mungu,MTBC Praise and Worship  na  Nathanaeli kutoka KCMC. Ni baadhi ya watakaohudumu.

Kumbuka ni tarehe 16 oct 2016 yaani leo hii saa 8 mchana katika moja ya ukumbi mkubwa na mzuri katikati ya jiji la Kilimanjaro uliopo UMOJA HOSTEL wahi na usichelewe hakuna kiingilio ni bure nenda ukakutane na nguvu za Mungu upate kuwa huru kupitia sifa na kuabudu. Zaburi 100 Mfanyieni BWANA shangwe,Dunia yote. Mtumikienii BWANA kwa furaha,njooni mbele zake kwa kuimba.

Share on Google Plus

About Desdery Charles

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.