NAMNA YA KUOMBEA NDOTO ZILIZOGUSA MAISHA YAKO (4&5)


Diana na Christopher Mwakasege
LENGO LA SOMO:
Kuimarisha Uhusino Wako Na Mungu Katika Kristo Yesu

JAMBO LA NNE  LA KUZINGATIA.-
Kuombea tafsiri ya ndoto husika kusikusahaurishe kuombea  Ujumbe ulio bebe ndoto hiyo.

Mambo Matatu ya kukumbuka

(1) Lengo la kuletewa ndoto ni kuletewa ujumbe.
Ayubu 33:14-15
Mungu anatumia njia moja wapo ya ndoto kusema na mtu au watu kutelemsha ujumbe

Pia fahamu. Hata kama chanzo cha ndoto sio Mungu, Mungu bado anaweza kutumia hiyo ndoto kukusaidia kwa kutumia ujumbe wa ndoto hiyo hiyo.
Torati 13:1-4

UKIFATILIA NDOTO VIZURI UTAGUNDUA VITU VIFWATAVYO

A) Kuna ndoto zilizo beba vitu vinavyoitaji tafsiri ili upate ujumbe ndani yake.
Mwanzo 40:5-23

Kuna ndoto zinavitu ndani yake ambavyo unaitaji utafsiri kwanza ndio utaweza kupata ujumbe ndani yake.

B) Kuna Ndoto ambazo zilizobeba vitu ndani yake ambayo maana yake ipo wazi havihitaji tafsiri ili kupata ujumbe wake.
Mathayo 1:18-24

Kuna ndoto nyingine haziitaji tafsisi vitu vilivyo ndani yake vipo wazi kabisa na ujumbe upo wazi

C) Kuna ndoto nyinge ambazo zina ujumbe peke yake hazijabeba vitu vingine zaidi ya ujumbe.
Mathayo 2:12,22

Kuna Doto zipo tofauti tofauti lazima uombe Mungu akusaidie katika kuzielewa.

(2) Omba Mungu akupe kufaham ujumbe wa ndoto, usiishie kufaham tafsiri yake peke yake. Daniel 4:4-19,27

Ulicho kiona ndani ya ndoto ni kibaya lakin kinaweza kugeuzwa.

Usiishie tuu kutafuta tafsiri ya hiyo ndoto na kujua maana yake ila ombea kujua maana ya ujumbe uliobebwa na hiyo Ndoto.

(3) Usipofanya Maombi ipasavyo ili ujue namna ya kushugurikia ujumbe wa ndoto ipasavyo, ujumbe huo unaweza kugeuka kuwa jaribu kwako.

Kama umeota watu wamevaa nguo nyeupe na wewe unawafata ila wao wanakukimbia basi jua ya kuwa Muda wako wa kufa umefika au umekaribia na Mungu anataka utengeneze ukiwa duniani (uokoke) kabla ya muda wako haujafika. Maana vazi jeupe ni vazi la wokovu.


KWA NINI MUHIMU KUFATILIA UJUMBE WA NDOTO

Ni kwa sababu ndani ya ujumbe uliomo ndani ya ndoto kuna taarifa ndani yake ili kukuandaa au kukuepusha na yaliopo mbele yako.

Mfano kutoka ktk Biblia kwa Yusufu mwana wa Yakobo.

Maisha ya Yusufu yalijengwa ndani ya ndoto saba nakati ya hizo ndoto mbili aliota yeye, nne alitafsiri na moja ilikuwa inajieleza yenyewe.

 • Ndoto ya kwanza na ya pili aliota mwenyewe.
  Mwanzo 37:5-11
   
 • Ndoto ya tatu mnyweshaji wa Faraho aliyekuwa gerezani.
   
 • Ndoto ya ya nne ni ya mwokaji mikate wa Faraho aliyekuwa gerezani.
   
 • Ndoto ya mbili zilizo fatta aliota faraho kwa usiku mmoja..
  Mwanzo 41,45
   
 • Ndoto ya saba ni ya baba yake Yusufu ambaye ni Yakobo.
 • Mwanzo 46:1-5

Linganisha na Zaburi 105:17-21

KUMBUKA.. Usipojua kuombea ipasavyo ujumbe uliopo dani ya ndoto ahadi inageuka jaribu.

Ujumbe uliopo ndani ya ndoto iliyo toka kwa Mungu ni neno lake Mungu kwako.

Kuna ndoto ambazo  Mungu atakupa, na ujumbe wake unaweza ukawa na maagizo ya kuweza kusubiri kwa muda mrefu ili hiyo ndoto iweze kutimia.

Kuna wakati ambapo watu wanakufanyia fujo ktk maisha yako ila sio tuu kwa sababu wanakuchukia ila ni kwa sababu wanawinda ndoto yako isije timia katika maisha yako.

Sio kila ndoto utatakayo ota unatakiwa kuwaambia ndugu zako au watu maana hao wanaweza kuwa adui kwako na wanaweza kukukasirikia, bali kuwa unaliombe tu.

Ndoto ambayo Mungu atakuotesha katika maisha yako lazima tuu itimie juu ya Maisha yako haijalishi unapitia magumu kiasi gani.

Hautakiwi kuwa na kinyongo juu ya ndugu zako au wale wanaokuchukia kwa kuota kwako.

Hautakiwi kumkasirikia Mungu wako pale unapokuwa unasubiri ndoto yako kutimia.

Kama wewe ni mwana wa Mungu na umepitia mateso mengi na majaribu unaweza kumwomba Mungu akayafipisha hayo mateso yako, wewe mtegemee Mungu.


VITU AMBAVYO VINAWEZA KUKUSAIDIA KUSUBIRI NDOTO YAKO 


Hakikisha ndani ya ndoto umepata Ujumbe (neno la Bwana lililopo ndani yake).

Maana yake utalipata kwa kutafuta ujumbe hutalipata kwa kutafuta tafsiri peke yake.

Uhusiano wako na Mungu  uchukuwe nafasi ya kwanza katika Maisha yako.

Kuwa na Neno la Mungu ndani yako maanalitakuwa ni chakula cha kukusaidia pale utakapo pitia mahali pagumu katika maisha yako.

Unapopata neno la Bwana na ukalichukua kuwa lako binafsi hilo neno linageuka kukuandaa kwa ajili ya maisha yako ya baada na kuwa nuru , uponyaji juu ya maisha yako.

Unapo anza kuomba juu ya ndoto zako mwombe Mungu akupe tafsiri ya neno kutoka kwenye Biblia kwa maana hakuna ndoto utakayo ota isiwe na tafsiri yake hata kama iyo ndoto imetoka kwa shetani.

Uhusiano wako na watu wanaokuzunguka.

Kama Mungu amekubebesha kitu  katika maisha yako huitaji kugombana na watu kwa maana nafasi ambayo Mungu amekuandalia ni ya muhimu sana kuliko kugombana na watu.

Nguvu za Mungu zitakazo kawa juu yako
Mithali 24:10

Ukisikia kuchoka au kukata tamaa siku ya jaribu au taabu wakati unasubiri wakati wa Bwana basi jua Nguvu zako ni chache. Nguvu ni Roho Mtakatifu ndani yako.

Unapokuwa upo kwenye jaribu unatumia Nguvu nyingi sana ndani yako hivyo unatakiwa uhakikishe unapata nguvu mpya. USIKATE TAMAA
Usikate tamaa maana wewe unaweza kuwakatisha au kuwasimamisha watu wengine wanao kuzunguka.

Mwl alifanya maombi kwa wale walio kata tamaa ili Nguvu za Mungu zishuke ndani yao kwa upya.Mungu akubariki sana


SEMINA YA NENO LA MUNGU UWANJA WA OTTU-MBEYA
SIKU YA TANO
TAR 14-OCTOBER -2016

LENGO LA SOMO NI KUIMARISHA UHUSIANO WAKO NA MUNGU KATIKA KRISTO YESU 

Kama ni mara yako ya kwanza unasikiliza masomo haya, nimekwenda kwa siku nne, na sina namna ya kurudi nyuma jitahidi pata kanda na sikiliza na kusikiliza hata kama ulikuwepo tokea awali pia pata kanda za masomo haya. Haya si masomo unaweza pata kirahisi sana maana si rahisi sana kufundishwa makanisani. Pia unaweza tembelea www.mwakasege.org kwa ajili ya kupata maelekezo wapi utapata kanda hizi hata kama uko mbali

Tuendelee na somo letu..

MUHTASARI

1 Usidharau wala usipuuzie ndoto uliyoota kwa maana ndoto ni lango mojawapo la kiroho

2 Vijue vyanzo vya ndoto na jua namna ya kuviombea ipasavyo.

3  Ng’oa kilichopandikizwa na shetani kupitia ndoto na madhara yake.

4 Kuombea tafsiri ya ndoto kusikuzuie kuombea na ujumbe wa ndoto husika.

5 Ombea Fikra zako zikwamuliwe mahali zilipokwamishwa kupitia ndoto ulizoota.

Kabla sijaenda mbali Zaidi kwanza tutazame maana ya maneno haya mawili muhimu.

Fikra  ni mkusanyiko na mtirirko wa mawazo yanayotengenenza msimamo wa kiutekelezaji ndani ya mtu.

Kufikiri  maana yake ni akili za mtu kulifanyia kazi wazo lilioingia akilini mwake.

VITU VITATU MUHIMU UNAHITAJI KUVIJUA

1 Fikra zinauwezo wa kutengeneza aina ya maisha na kiwango chake
Mithali 23:7a maana aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo, na kuna tafsiri zingine zinasema

 • Maana atafakarivyo
 • Maana awazavyo
 • Maana afikirivyo

Kwahiyo aina ya maisha uliyonayo ni matokeo ya unavyotakari.
Ili kujua kutafakari au kufikiri kwa mtu angalia aina ya maisha, maana nikihitaji kujua unatafakari nini maishani mwako au unafikiri nini maishani mwako naangalia aina ya maisha unayoishi ndiyo tutajua unachotafakari.

Biblia inasema aonavyo nafsini mwake, haijazungumzia kuona mwili au rohoni bali inazungumzia kuona nafsini. Katika uumbaji wa Mungu, Mungu aliumba roho kwanza na ndipo akaumba mwili na alipopulizia pumzi ndipo mtu akawa nafsi hai.  Kwa hiyo kwa itifaki ya Mungu uumbaji unaanza na Roho unakuja mwili alafu nafsi. Kwa hiyo mtu ni roho anayo nafsi anaishi kwenye mwili. Sasa kaz ya nafsi ni kutafsiri kutoka kwenye roho kwenda kwenye mwili na kutoka kwenye mwili kwenda kwenye roho. Nafsi yako ikivurugwa unakuwa na hali ngumu sana. Ndio maana Daudi alisema nafsi yangu mhimidi Bwana ina maana nafsi yake ndiyo inatakiwa imhimidi Bwana na sio mwili au roho.
Na Pia Zaburi 84:2 Nafsi yangu imezionea shauku nyua za Bwana, Naam, na kuzikondea. Moyo wangu na mwili wangu Vinamlilia Mungu aliye hai.

Mwili unaenda kwa kuona, na Roho inaenda kwa Imani kwa hiyo nafsi kazi yake ni kutafsiri yaani kutoa kwenye imani na kuleta kuona halisi kwa njia ya mwili. Kwa sababu kwenye nafsi kuna akili za kufanya kile kilichonekana kwa imani kiwe halisi kabisa.  Lengo la Mungu ni kumfanya mwandamu aweze kuishi kwenye ulimwengu wa roho na wa kimwili kwa wakati mmoja.

Ndiyo  maana ni mwanadamu peke yake mwenye sifa ya kuishi katika ulimwengu wa mwili au wa roho. Hata Mungu akihitaji kuwa Duniani ni lazima avae mwili huu wa damu na nyama. Utanielewa kwanini Yesu ilibidi aje katika ulimwengu huu achukue mwili kwa Mariam. Mungu mwenyewe ndiye kapewa hadhi hii ,malaika hawana na hadhi hii ya kumwingia mwanadamu. Ndio maana hata shetani nae anatuma mapepo na kuwaingia watu. Maana ili uweze kufanya kazi katika ulimwengu huu mwili unahitajika sana. Bila mwili hamna kinachoendelea hapa duniani.

Dhambi ilipoingia iliua roho na mwili ukawa uanenda kivyake na roho ilipoteza mahusiano na mamlaka yake ndiyo maandiko yanasema roho I radhi lakini mwili ni dhaifu. Hii ni kwa sababu ya dhambi ilivuruga utaratibu wote . Dhambi ni uasi hii unaipata kutoka 1 Yohana 3:4  maana ya uasi ni kwenda kinyume cha., kwa hiyo baada ya dhambi kuingia nafsi ikawa inafanya kazi kinyume cha mapenzi ya Mungu.

Nafsi ilipewa jukumu la kutengeneza aina ya maisha na viwango vyake sawasawa na neno la Mungu linavyotaka. Hili somo la Fikra ni pan asana, Tafuta kanda za Dar es Salaam za Sept Mwaka huu, hili somo la Fikra nilifundisha kwa siku nane, na sikumaliza  ooh Hii ni siri muhimu sana unahitaji kujua.

2. Mungu au shetani wanatumia ndoto ili kugusa fikra za mtu


MFANO 
Mathayo 1:18-20 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu

Biblia inasema alipokuwa anafikri hayo aliota ndoto, rudia tena mstari huu hadi uone ninachotaka uone hapa Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
  
Yaani alipokuwa anafikiria kumwacha Mariam kwa siri ndipo alipoota ndoto usiku wakati amelala. Sasa hii ndoto ilikuja kujibu alichokuwa anafikiria. Na nimekuambia kufikiria ni kulifanyia kazi wazo lililoingia akilini mwako na wazo alilokuwa nalo ni la kumuacha Mariam. Ina maana wazo lililoingia liliweka msimamo Fulani ndani yake wa kumuacha Mariamu, ndiyo maana Mungu ilibidi aweke na mstari kabisa ili kuwa ni yeye ‘Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema,’  (Isaya 7:14) Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi. Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe; (Mathayo1:23-24)

Kwa sababu kwa hali ya kawaida ni ngumu kuamin kuwa ni  kwa uweza wa roho mtakatifu ndiye kafanya Mariam apate ujauzito maana hili suala ni jipya na halijawahi kuokea hata siku moja.

kwa sababu Yusufu alijua kuwa kama atasema ile mimba siyo ya kwake lazima Mariam angeuawa kwa kawaida ya Dini ya Kiyahudi. Sasa ile kuona Mariamu asiuawe Yusufu aliazimia kutoroka ili akubali kubeba ile aibu ionekane ni yeye aliyempa mimba. Na wakati anawaza hayo ndipo Malaika akamtokea katika ndoto. Na asante Yesu alitii ile ndoto, sasa fikiria asingetii ile ndoto na angesema hii ni ndoto tu kama Farao alivyosema unafikiria ingekuwaje.


Hapa ndipo utaelewa ile Ayubu 33:14-19 ‘’ Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani; Ndipo huyafunua masikio ya watu, Na kuyatia muhuri mafundisho yao, Ili amwondoe mtu katika makusudio yake, Na kumfichia mtu kiburi; Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga. Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake;

Soma pole pole hiyo mistari hasa niliyowekewa nyota na Linganisha na  Mathayo 1:18-20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu_

Kwa hiyo unaweza ukawa unawaza juu ya jambo Fulani na usiku ukaota ndoto na fuatilia vizuri hiyo ndoto iliyokuja  maana usiishie tu kupata tasfir yake bali na ujumbe maana ujumbe utakupa cha kufanya, na hutua zake ambazo unatakiwa uzifuate. Na kipingele hiki naona msisitizo sana ni kuwa soma kwa kupata maarifa masomo haya

Tuko pamoja mpaka hapo? Kama hujaelewa rudia tena soma hadi uone kitu Mungu anataka uone, kama bado nyunyiza damu ya Yesu katika somo hili na Yesu afungue Fikra zako uweze kuelewa. Ooh Mungu wangu akupe kuelewa afunue akili zako ili uweze kuelewa maandiko haya.


Sasa suala la umuoe nani au uolewe na nani ni suala la akili yako na nafsi yako siyo suala la Roho yako
Ngumu eeeh ngoja nikupe mfano

Kuna wakati Fulani dada mmoja alikuja nyumbani kwetu akatukuta mimi na mke wangu alikuja nyumbani kutushirikisha suala la yeye kuolewa na akatuletea na jina la huyo kijana, maana alisema naomba mnisaidie kuomba kwa Mungu kwa sababu mimi nimejaribu kufikiria ila naona kama sielewi hivi. Basi tukamwambia sawa tutaomba. Basi haikumalizika wiki  usiku mmoja niliota ndoto  nikaona yule dada na yule kijana wako nyumba moja tayari na baada ya muda yule kijana aliondoka bila taarifa. Basi nikaomba Mungu anipe tafsiri na ujumbe.

Tafsiri Yule msichana tayari alikuwa kafanya maamuzi tayari ya kuolewa na kijana na ndio maana nilmuona yupo kwenye nyumba moja na kijana. Lakini ni kuwa ile ndoa yake anayotaka kuingia haitadumu kwa muda mrefu.
Ujumbe Yule Kijana sio wa kwake kwa hiyo inabidi aachane nae tu. 

Baada ya kumuambia hivyo yule msichana akasema jamani naomba mniombee tu. Bassi baada ya hapo alioondoka hatukumuona tena na tulipomuona alikuwa tayari na kadi ya harusi ya kuolewa na Yule kijana. Na sisi tulisema alichosema Mungu ni hiki basi kwa kuwa wewe umeamua basi sisi tutakusndikiza tu. Ila ujue gharama iko, Basi wakaoona na wakazaa na mtoto baada ya muda kidogo Yule kijana alitoweka Nyumbani bila maelezo. Sawa sawa na ile ndoto niliyoota.


Kijana sikia kuwa makini sana kwa sababu unakuta  akili yako inaanza kuishi na mtu tayari wakati mkiwa wachumba bado na unaishi nae miaka kadhaa  ijayo akilini na sasa ghafla unaota  ndoto Mungu anakuambia sio yeye ghafla na wewe unaanza kupata  tabu kidogo. Sikuambii kuwa hamna dhoruba katika ndoa hata kwa watendaji wa neno. neno la Mungu liko wazi kabisa linasema kuwa dhoruba itakuja kwa kila mtu ila sasa mwisho wake itakuaje, hapo ndipo pana tofauti kati ya kuwa mtendaji wa neno na asiyekuwa mtendaji wa neno

Mfano kidogo alioupata Yusufu na jaribu gumu kuliko unavyofikiri maana ni jambo zito sana alilolipitia Yusufu. Inahitaji sana hekima ya Mungu na kuwa mtii wa kile Mungu anataka kukuambia. Fikiria Yusufu angetoroka pole pole ingekuaje kwa Mariam. Lazima angeuawa na je kama angeuawa Yesu angezaliwa wapi? Ooh kijana mtii Mungu katika maamuzi yako.


Sikiliza msichana akija kijana kwako anataka kukuoa na una Yesu moyoni awe tayari kukuchukua wewe na Yesu wako na asiseme mweke Yesu wako pembeni. Gharama ya kuingia kwenye ndoa bila Yesu ni gharama kubwa saba. Heri Kijana akae Pembeni lakini Yesu wako abaki. Na ndio maana watu wengi wakitaka kuolewa/kuoa  Mungu anasema nao kwa njia ya ndoto na hawajui

MFANO WA 2

Daniel 4:2,5,19 Mimi nimeona vema kutangaza habari za ishara na maajabu, aliyonitendea Mungu aliye juu, Nikaota ndoto iliyonitia hofu; mawazo niliyokuwa nayo kitandani mwangu, na njozi za kichwa changu, zikanifadhaisha. Ndipo Danieli, aliyeitwa jina lake Belteshaza, akashangaa kwa muda, na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akajibu akasema, Ee Belteshaza, ndoto ile isikufadhaishe wala tafsiri yake. Belteshaza akajibu, akasema, Bwana wangu, ndoto hii iwapate wao wakuchukiao, na tafsiri yake iwapate adui zako


Ndoto iliyoingia ilitengeneza msimamo Fulani na Daniel alipopewa hiyo ndoto nae pia ilimfadhaisha. Lakini Mungu alikuwa anafuatilia msimamo wa Nebukadreza baada ya kumpa ujumbe wake.  Lakini cha ajabu Nebukadreza hakukubaliana ili kubadilisha msimamo wake lakini hakubadilisha  na alikuwa na allowance ya miezi 12 ili yamkini afanye toba hakufanya Toba na hata Daniel nae hakumuombea Toba kwa Mungu  na ona matokeo yake aligeuzwa Fikra zake akawa kama Mnyama kwa Nyakati 7.

Mungu au shetani wanatumia ndoto kugusa maisha ya mtu

Mithali 3:1-5 Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu. Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani. Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu. Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe

Mungu katuruhusu kutumia akili zetu na sio kuzitegemea ila kuzitumia aaah ni ruksa kabisa lakini kuweka tegemo kwake ndio makosa.Akili ziko kwenye nafsi, na jua kuwa akili hazikuumbwa ili zifanye kazi peke yake  ila zinatakiwa ndani yake ziwe na ufahamu wa Kimungu ili kuweza kuishi maisha ambayo Mungu anataka. 2 Wakorintho 4:3-4 Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu

Ibilisi ndio anapokuwa anawinda maisha  yako anakuja moja kwa moja fikra zako na kuzipofusha. Na sababu ya yeye kuzipofusha ni kwa ajili yake ili usione fikra zake mbaya zikiingia.  2 Wakorintho 2:11 Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake. Shetani alipoenda kwa Hawa aliingia kwenye Fikra zake na akazipofusha na ndipo aliweza kumdanganya.  Maana biblia inasema 2 Wakorintho 11:3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.

Pia angalia Warumi 1:28 ‘’ Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. Kwa hiyo ukimkataa Mungu katika fahamu zako ujue kuwa atakuacha ufuate mambo yasiyofaa na gharama yake ni kubwa sana.

>>Mungu hulituma neno lake, na mawazo yake Isaya 55:8, 11 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana. ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.
Kwa hiyo kuna uhusiano kati ya neno na njia na njia maana yake ni mkakati wa kukutoa mahali ulipo kwenda mahali pengine yaani hatua ndio maana neno linasema hatua za mtu zaimarishwa na Bwana Mithali 19:6, Zaburi 37:23.

3 Ndoto inaweza kutumika kufanya fikra zako kufungwa au kufunguliwa maisha yako
Daniel 4:31-37 Hata mwisho wa siku hizo, mimi, Nebukadreza, nikainua macho yangu kuelekea mbingu, fahamu zangu zikanirudia; nikamhimidi Yeye aliye juu, nikamsifu na kumheshimu Yeye aishiye milele. kwa maana mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi hata kizazi; na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe? Basi wakati uo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi. Basi mimi, Nebukadreza, namhimidi Mfalme wa mbinguni namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili 

Daniel 4:15-16 Walakini kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikapate maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama katika majani ya nchi; moyo wake ubadilike, usiwe moyo wa binadamu, na apewe moyo wa mnyama; nyakati saba zikapite juu yake.


SASA ONA TAFSIRI YA NDOTO.

Daniel 5:18 – Hapa unapata tafsiri ya ndoto aliyoota Nebukadreza.  Na ukiunganisha na Daniel 4 ni ushuhuda wa Nebukadreza jinsi alivyopita kwa miaka 7 alipokuwa Mnyama na ufalme wake kurejeshwa. Alikuwa amenyang’anywa ufalme wake na Mungu. Na Mungu ndiye aliyempa ufalme Nebukadreza lakini yeye alienda kinyume na yeye alieuziliwa kwa amri ya walinzi lakini aliyemtoa ni Mungu mwenyewe.


Baada ya kupewa ufalme alianza kujiona yeye ndiyo yeye na akawa anafanya mambo kama yeye anavyojisikia. Lakini Mungu aliyempa alimuezua na hakuishia hapo aliondoa na ufahamu wake akawa kama Mnyama. Na kwa kuwa alimkataa Mungu katika fahamu zake basi Mungu akaziondoa aakili zake na kamauacha afuate akili zake zisizofaa. Kipindi cha miaka 7 kilisimamisha kabisa maisha yake na zilimpa aina Fulani ya maisha  na kwa kuwa alipewa allowance ya miezi 12 ili yamkini afanye toba hakufanya Toba,na baada ya meiz 12 kupita ndipo alipoezuliwa maana ule muda ulikuwa umepita wa kufanya Toba.

Swali  Je aina ya maisha unayoishi au kiwango cha maisha unayoishi ndicho Mungu alikukusudia. Kama sio ukigundua kuwa sio hicho basi ujue kuwa fahamu zako zinakurudia kwa sababu umegundua ila kama hujui basi fahamu zako zimekamatwa

Ni kweli kabisa umeokoka na mbinguni utaenda ila cheki maisha yako yamechakaa, na hawa watu wakikutazama na ukijifananisha nao huna tofauti n tofauti yako ni kuwa una Yesu moyoni. Sasa ni kazi yako kujua kuona agano la Mungu linasemaje na je unayoyasoma yapo wenye maisha yako?

Sasa chukulia wewe ni Nebukadreza na umeota kuna pingu na kisiki kimekatwa. Na kwa kuwa hujui maana yake nini na chakufanya hujui unajikuta unakemea kuanzia asubuh hadi jion kwa sababu hujui kuwa ulitakiwa utubu maana hujajizoeza kuomba tafsiri kwa Mungu ili akusaidie kujua maana ya ujumbe wa ndoto unakuta ndoto hiyo umeshindwa kudaka kilichoka ndani na maisha yako yanakuwa magumu sana.

Pia kwa kuwa hujui unakuta umeota ndoto mbuzi kafungwa kwenye mti nakamba, na wewe unajua ni mbuzi  kawaida kumbe ni wewe umefungwa ni sawa na Nebukadreza hakujua sawa sawa maana ya ile ndoto na hakutilia maanani na ona alipelekwa msituni.

Sasa kama hutaki kufuata mfumo wa Kimungu itakuwa hasara sana kwako, na ndio maana unaweza ukawa na fedha lakini ukawa mlevi na unaweza ukawa na akili sana lakini bado maisha yako yakawa mabovu bila Mungu akili yako haina faida, ni sawa na injini ya Petroli ukaweka Diesel  uwe na uhakika tu kuwa haifiki mbali.

UTAFANYAJE KUJUAKUWA UFAHAMU WAKO UMEHARIBIKA NA UNAHITAJI KWENDA HOSPITALI YA MUNGU


Tutatumia mfano wa Nebukadreza.

1. Alipoteza kujitambua kwa miaka 7

 Ndipo aligundua kuwa Fahamu zake zilipotea ndipo alijua. Ukiona maisha yako hayafai kuishi ujue kuwa unahitaji kwenda kwa Mungu ili akusaidie maana kipimo cha maisha yako ni agano.

2. Cheki watu wanaokuzunguka wakati huu na husaidiki japo wanajithaidi kukusaidia husaidiki
Nebukadreza unadhani ndugu zake walikuwa hawammpendi, tena kiongozi wa nchi unadhani ilikuwa ni rahisi tu kwenda msituni. Lazima walimsaidia ila waliona hasaidiki na wakaamua kumuacha aende porini. Na ni sawa na wewe unakuta watu wamekukariri kuwa yule yule mwenye matatizo kaja tena.

3. Cheki waliozoea kukutembelea tena wako wapi


maana biblia inasema utajiri huleta marafiki. Lakini ona ufahamu wa Nebukadreza ulipopotea ulipoteza na marafiki na uliporudi watu wote waliokuwa wanamzunguka fahamu zao wote wailirudi.
Yamkini angejua wakati Mungu alipozungumza nae kwa njia ya ndoto lakini alipuuzia, na gharama yake ilikuwa ni Kubwa sana.

Ukisoma waebrania 4:1-4 Kikwazo cha wana wa Israel kwenda Misri ilikuwa ni kwenye Fikra zao maana unaweza ukawa na imani na ni sawa kabisa lakini ukishindwa kuchanganya imani yako na Fikra zako unaweza ukaishia jangwani na kanani yako huwezi fika.

Watu wengi ndoto zao zimekufa kwa kushindwa kuchanga Fikra yaani kutumia akili zao na Imani zao Na ukimkaribisha Mungu atakusaidia sana maishani mwako na Mungu atakuletea fahamu kwa upya na kukubadilisha.

Nakumbuka nyakati zile Mungu ananionesha kuwa ntakuwa nahubiri kwenye uwanja wa mpira kama hivi ilikuwa ni ngumu sana kuamini maana kupata tu watu 100 ilikuwa ni kazi na nikaona nisomee uchungaji na Mungu alinitoa kwenye nia yangu mbaya  maana nilikuwa sina mpango wa kuwalea ila nilikuwa ntafuta watu.

Ooh ni neema iloje mtu wa MUNGU, Nebukadreza alipewa miez 12 ili aombe lakini hakuomba na Daniel pia nae hakumuombea Toba Nebukadreza. Leo neema ipo hapa shikilia hili wingu omba kwa Mungu,

Baada ya hapo Mwl alituongoza kwenye maombi mazuri sana wewe fanya kwa imani omba na naamini Mungu atakupa hitaji lako ng’ang’ana na Mungu wako. Kumbuka kuombea semina hizi na njia ambazo Mungu anazitumia kukufikia. Ubarikiwe sana.

Kusoma Zaidi Mafundisho ya Mwl Mwakasege tembelea

FACEBOOK
https://www.facebook.com/Christopher-Diana-MwakasegeMana-Ministry-132462780111984/

Youtube
https://www.youtube.com/channel/UC4p4lrpgpNd-9bHPgHJ4xWw

Ustream
http://www.ustream.tv/channel/mwakasegemanaministry

Tocuti
www.mwakasege.org

Na kama umeokoka kupitia mafundisho haya soma somo la Utangulizi katika link hii http://www.mwakasege.org/mafundisho/hongera/utangulizi.htm

Glory to God Glory to God.
Felix….      
+255716918848.

Share on Google Plus

About Elie Chansa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.