TAMASHA KUBWA LA MUZIKI WA INJILI KUFANYIKA KESHO CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM


Hapo kesho katika viwanja vya chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) kunatarajiwa kufanyika tamasha kubwa la muziki wa injili, litakalozikutanisha kwaya kongwe na mashuhuri za kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania, Dayosisi ya mashariki na pwani kwa jimbo la Magharibi.

Tamasha hilo ambalo linafanyika siku ya Nyerere Day lipo chini ya umoja wa kwaya za Uinjilisti na Uamsho jimbo la magharibi almaarufu kama UKUU litakuwa na kiingilio cha 5000 kwa mshiriki linatarajiwa kuwa la siku nzima kuanzia asubuhi majira ya saa 3 hadi saa 12 jioni.

Kati ya kwaya zitakazoshiriki ni pamoja na Uinjilisti Kijitonyama, Uinjilisti Safina Magomeni, Uinjilisti Sayuni Kinondoni, Uinjilisti Tumaini Msasani, Uinjilisti Tumaini Kawe, Uamsho Amkeni Kinondoni, Uamsho Kijitonyama, Uinjilisti Boko na nyingine nyingi zaidi ya 15. Ambapo mchungaji Lewis Hizza ndiye atakayekuwa mwenyeji wa kuzikaribisha kwaya hizo, ambazo hufanya tamasha mara mbili kila mwaka.Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.