MY PRAISE CONCERT NDANI YA UMOJA HOSTEL KILIMANJARO OKTOBA 16

                        
The Heaveanly Melodies ni moja ya kikundi kinachofanya vyema kwa ukanda wa Kaskazini hasa kwa namna ya kipekee, wanapohudumu lakini pia kwa namna ambavyo wanaushusha uwepo wa Mungu na kuhakikisha watu wanahudumiwa na Mungu kisawasawa kupitia huduma yao ya uimbaji.

Baada ya kuhudumu sehemu mbalimbali na kwenye matukio makubwa ambayo yameshawahi kujiri mkoani kilimanjaro ikiwemo moja ya huduma kubwa kwa Afrika iitwayo Sacrifice of Praise Africa (SOPA) na nyinginezo nyingi zote kwa mwaka huu wa 2016 wameamua kuja na yao sasa ambayo tayari imeshawahi kufanyika mwaka jana na watu walikutana na Mungu kwa namna ya kipekee sana.

My Praise Concert ni huduma ambayo ina lengo la kuwakutanisha watu wote ili wamsifu Mungu na kukutana na Mungu kulingana na Neno la Mungu linavyosema, Mungu anaishi katika sifa. Hivyo basi tukio hili limeandaliwa ili kwa pamoja na wengine, uweze kumsifu Mungu kwa nguvu zako zote kadiri uwezavyo kwa muongozo wa neno la Mungu kutoka Zaburi 19:1

Tukutane Jumapili ya tarehe 16 Umoja Hostel ndani ya Jiji la Moshi, Kilimanjaro.

Share on Google Plus

About Desdery Charles

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.