WAPENZI WA JOYOUS CELEBRATION KAENI MKAO WA KULA DVD NAMBA 2 KUACHIWA KARIBUNI

Joyous Celebration wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kurekodi DVD no 19 Soweto mwaka juzi.
Kundi la Joyous Celebration linatarajia kuachia DVD nyingine kabla ya mwaka huu kuisha, ikiwa na nyimbo za zamani zilizoimbwa na waimbaji nguli waliomaliza mkataba na kundi hilo wakati wakisherehekea miaka 20 ya kundi hilo, sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Moses Mabhida jijini Durban mwezi Disemba mwaka jana, Gospel kitaa ikiwa kati ya malefu waliohudhuria tukio hilo.

Wakati wa tukio hilo Joyous ya sasa na waimbaji wa zamani kwa ujumla waliimba nyimbo zisizopungua 72 hata hivyo DVD iliyotolewa awali mapema wakati wa pasaka mwaka huu, ilikuwa ya nyimbo mpya kutoka kwa waimbaji waliopo kundini mpaka sasa, lakini sasa kundi hilo linapanga kuachia DVD part 2 zikiwa nyimbo zilizoimbwa na waimbaji hao wazamani uwanjani hapo.

Kwasasa Joyous inakamilisha mazoezi yake tayari kuelekea nchini Marekani katika jimbo la Dallas kurekodi DVD na CD yao ya 21 ambako watakuwa wenyeji wa Askofu TD Jakes katika kanisa la The Potter's House. Licha ya kurekodi album mpya lakini pia kundi hilo litafanya ziara katika majimbo mengine nchini Marekani zaidi ya matano kabla ya kurejea nchini Afrika ya kusini.


Nginde Nginde kutoka kwa Mkhululi Joyous 20Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.