NGOBEKEZELA NDIO CHAGUO LA GK KUTOKA KWA GWIJI WA INJILI ALIYELALA MAUTIKatika chaguo la GK hii leo tupo na gwiji wa muziki wa injili Afrika ya kusini aliyelala mauti miaka kadhaa iliyopita kwa ugonjwa wa kansa ajulikanaye kwa jina la Vuyo Mokoena, mwimbaji ambaye uimbaji wake ulitokea kuwabariki wengi nchini mwake na nje ya nchi hiyo. Ukaribu wake na malkia wa muziki wa injili Rebecca Malope ulisababisha baadhi ya watu kudhani ni mapacha kitu ambacho hakikuwa cha kweli. Hata siku chache kabla ya mauti yake Vuyo aliandika wimbo maalumu ambao angependwa uimbwe kwenye mazishi yake na kutaka wimbo huo uimbwe na Rebecca ambaye alifanya hivyo.

Leo kupitia gwiji huyu ambaye kazi zake bado zinaendelea kubariki na kuponya mioyo ya wengi tumekuchagulia moja ya wimbo wa kuabudu wa nchini humo ambao aliurekodi miaka kenda nyuma ujulikanao kama 'Ngobekezela' ambao pia waimbaji wengi nchini humo wameurekodi akiwemo mwanadada Puleng March aliurudia tena akiwa na Joyous Celebration ambako Vuyo pia alitumika kwa karibu na rafiki yake pastor Jabu Hlongwane. Tunatumaini wimbo huu utafanyika baraka kwako jumapili ya leo. UbarikiweShare on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.