SOMO:NAMNA YA KUOMBEA HALI YA KIROHO YA ARDHI ILI UFANIKIWE KIMAISHA (2&3)

SEMINA YA MWL CHRISTOPHER MWAKASEGE(MANA MINISTRY)-IRINGA:

LENGO: Kujifunza mbinu za kuomba ili hali ya kiroho ya ardhi iliyokwamisha mafanikio yako iondoke ili uweze fanikiwa.
HATUA  ZA KUFANYA ILI UONDOKE HAPAO ULIPO AU UMWOMBEE MTU ALIYEKUJA KUOMBA MSAADA UMSAIDIE KUTOKA HAPO.

1.PELEKA OMBI HILO KWA MUNGU.Usijaribu msaidia huyo mtu au kujisaidia bila kumuuliza Mungu kwasababu wewe huna jibu la matatizo  yake bali kwasababu una mahusiano mazuri na pale anapotaka maombi yake.ZABURI 107:19-20.Wana wa Israeli walipoenda kinyume na Mungu walimlilia Musa na yeye pia akamlilia
Mungu.

2.POKEA NENO LA MUNGU UNALOPEWA NA MUNGU KWA AJILI YA HUYO ALIYEKUOMBA UMWOMBEE AU UJIOMBEE.ZABURI 107:17-20.
Unajiuliza unafanyaje?Mungu anakuletea NENO ISAYA 55:11.Ukitaka kufanikiwa kwa mpango wa Mungu lazima upokee NENO.YEREMIA anasema Neno la Bwana likanijia likasema".Kwa hiyo ni lazima usikie Neno la Bwana sio lako.

3..OMBA MUNGU AKUPE KUSIKIA MUONGOZO WAKE KWAKO KUTOKA KWENYE NENO ULILOPEWA.RUMI 10:17.
Imani huja kwa kusikia.Lazima ujue utaratibu Mungu alionao katika kukufanikisha.Imani chanzo chake ni kusikia kwa NENO LA KRISTO.
Mungu anaweza sema na wewe kupitia mistari iliyopo kichwani mwako,kusoma Biblia,CD,kipindi cha redio au Runinga ambako huwa kuna Neno ameliweka huko ili upate sikia ujumbe wake.
Ni lazima uchimbe historia ya huyo mtu au ikiwa ni wewe ili kufuatilia hiyo hali anayolalamikia kutokufanikiwa kwake au hali inayofanya kutokufanikiwa kwako.2FALME 24:1,8-10 23:36-37.Mungu atakupa maarifa jinsi ya kujihudumia wewe au mwingine.Umejua ni adhabu ya ukoo wapi ni lango ya dhambi hiyo.Wakiendelea kukalia KITI cha DAUDI adhabu itaendelea kukufuata inabidi usikae ili utoke.Kama kuna Kiti cha ukoo,familia,taifa umekalia usipotoka hapo atakuja mwingine mwisho utarudi pale pale au utatenda yale yale.
Yehoyakimu alikaa miezi 3 akaondolewa na baada ya miaka 3 akaasi akawa chini Nebukadreza(Shetani).

4.OMBA TOBA KWA AJILI YA DHAMBI  ZA MAOMBI ALIYOLETA YULE MTU AU YAKO KWASABABU YA UOVU WA WAZAZI AU WATANGULIZI ULIVYOSABABISHA WASIFUATE MAAGIZO YA MUNGU.YEREMIA 22:21.
Sio kutubu tu bali kujua mahali dhambi ilipoingia(ujana wa wazazi wao au wako),mlango wa kutokumsikia Mungu DANIELI 6:19.KUTOKA 20:5.
Mungu hapatilizi dhambi bali uovu.Kuna tofauti kati ya DHAMBI na UOVU.DHAMBI ni uasi-kwenda kinyume na maagizo ya Mungu(unatumia vitu kinyume na alivyokuagiza).UOVU ni udhaifu.
Tunatubu kwa ajili ya dhambi zetu na uovu wa babu zetu.Unaweza kwenda jela kwasababu hakukuwapo mtu wa kutetea kisheria katika lile kosa na si kwasabau umetenda dhambi.Dhambi maana yake unatumia vitu ulivyopewa kinyume na utaratibu.Mungu hapatilizi dhambi bali udhaifu,ule udhaifu unaacha kukusaidia.Wote tumetenda dhambi na kukosa utukufu wa Mungu.Udhaifu ni hali inayokaa kwenye mwili,nafsi,roho na kujenga mazingira uzao wako uliotoka kwa babu au baba.Huzaliwi na dhambi ya kunywa pombe bali udhaifu, huwezi stahimili hali hiyo,ukisikia harufu ya pombe huwezi stahimili.Kwanini utubu dhambi? ili Mungu aingilie kati ili uasi usiendelee.Mungu aingilie kati uovu, ili udhaifu huo usiendelee kwa watoto wako.Ni lazima ufute kisheria ili utoke hapo.

5.FUTA AU ONDOA LAANA KATIKA ARDHI KWA KUTUMIA DAMU YA YESU.YREMIA 22:29-30.
Ardhi imeandika na kutunza kumbukumbu. WAEBRANIA 9:19-24.
Damu ya YESU inaondoa na kufuta dhambi.Damu ya Yesu inaonekana kwa ajili ya mtu unayemuombea au wewe na kutaka kumsaidia.Mbinguni kuna nakala mbili.!.Nakala za makosa yako mbinguni 2.Nakala za mashtaka ya shetani kwa Mungu.
Damu ya Yesu inakuja kufuta mashtaka yote lakini kwenye ardhi yapo.Unasema nafuta maneno yote ktk ardhi yanayofanya nisifanikiwe.Ardhi imetumika kama polisi na magereza maana kesi haiwezi kwenda mahakamani kama nakala ya kesi haipo.Ardhi imeiumbiwa ikuzie kama hati,ardhi itakapoona Damu imekuja na Jina la Yesu itafuta mashitaka yote.Nebukadreza alipata nguvu toka ardhi kuwatesa wana-Israeli.

6.LAZIMA UKEMEE ROHO AMBAYO INAYOZUIA MAFANIKIO.
Kemea mzaingira ya uasi,kemea roho ya UKIWA kwasababu unaishi kama umenyang'anywa kitu(Mume,kazi,mke,uchumi,gari,biashara n.k)Kazi ya roho ya ukiwa ni kukunyang'anya uwe mikiwa,uwe na hali ya upweke.KOLOSAI 1:13-14.
Yesu anaachilia Damu na kukumboa na anaachilia hati ya kukumboa kutoka hali hiyo.

7.MWOMBEE HUYO MTU AU JIOMBEE WOKOVU NA UTII KWA MAAGIZO KWA MUNGU ATAKAYOKUWA ANAMPA/ANAKUPA NA AGANO LAKE. YEREMIA 22:29.
Maombi hayakufanikishi bali NENO toka kwa Mungu(sio kuendeda kila mkutano ukaombewe tu bali uwe unaomba Mungu akupe Neno toka kwake la kukukusaidia).
Ukitaka mafanikio Mungu anakupa Neno ili uwe msikivu kwa kukupa mawazo ili usikwame.

8.OMBA MUNGU AKUONDOLEE HALI YA UKIWA KATIKA NYUMBA YAO AU YAKO ARUDISHE KITU KITAKACHOKUONDOLEA UKIWA.
Dunia ilipokuwa ukiwa kuna kitu Mungu alikirudisha.Akikuondoa kwenye NAFASI huacha hali ya ukiwa.Habili alipouwawa hali ya ukiwa iliingia kwenye familia ya Adamu,vizazi saba mpaka Seth alipozaliwa alirejesha hali ya faraja kwasabu kuna kitu Adamu alikuwa amekosa Seth alikirejesha(Kumcha Bwana)
Mfao kwenye familia atakapopatikana mtu mmoja awe mtoto,mjukuu au kilembwe ambaye amebeba kitu flani cha wazazi ambacho wanakipenda iwe biashara,uchaji wa Mungu,uongozi n.k faraja hurejea katika familia Yeremeia 22:5

9.ISEMESHE ARDHI NA MBINGU KWA UPYA VISIKWAMISHE MAFANIKIO YAKO AU YAKE.KUMB LA TORATI 31:28-30, 30:19-20 32:1.
Unafanya hivyo ili ardhi na mbingu zitunze kumbukumbu na maneno utakayosema ili baadaye pasiwepo na cha kukukwamisha/kumkwamisha mafanikio yako/yake.

3⃣
LENGO:Kujifunza mbinu za kuomba ili hali ya kiroho ya ardhi iliyokwamisha mafanikio yako iondoke ili uweze fanikiwa.
Ikiwa mtu amekuja kwako kuomba msaada wa maombi kwasababu hafanikiwi au wewe mwenyewe hufanikiwi ktk ujenzi unaotaka kujenga au aliokwisha anza kujenga au umekwama mahali unataka kumalizia fedha zinapotea.Unamuombaje au unamuombeaje?.
HATUA ZA KUFANYA ILI UTOKE AU ATATOKE HAPO.
1.PELEKA OMBI HILO KWA MUNGU.
Kwasababu jibu huna bali kwasababu ya mahusiano uliyonayo na Mungu unaye mwamini wahitaji mpeleka kwa Mungu.
2.POKEA NENO LA MUNGU KWA AJILI YA HUYO ALIYEOMBA UMUOMBEE AU KWA AJILI YAKO.
ZABURI 107:19-20,ISAYA 55:11.
Neno la Mungu lina wazo na mikakati ndani yake inayotoa mvua mvua na kunyesha ili kumea NENO la kukusadia ktk kukufanikisha.
Nchi inaweza kuwa na WAOMBAJI wazuri ila kama hawana NENO ni ngumu sana kufanikiwa.Unaomba mvua inanyesha lakini hujaandaa MBEGU ni vigumu kustawi.Ni lazima na ni sheria ya KI-MUNGU kupokea Neno ili ustawi.
3.OMBA MUNGU AKUPE KUSIKIA MWONGOZO WAKE KWAKO KUTOKA KWENYE NENO ULILOPEWA NA MUNGU ULIPOMWOMBEA HUYO MTU AU WEWE.RUMI 10:17.
Ni lazima usikie Sauti ya NENO ambayo hutengeneza uhakika(IMANI) ili kufungua macho ya imani kuona kila linalotarajiwa.Ebr 11:3.
Imani huja kwa kusikia.UTasikiaje? Kwa jinsi linavyokuja.KUMB LA TORATI 8;7,11-12.Kuna suala la umiliki wa ardhi kiroho na kimwili,kabla ya umiliki wa kimwili lile eneo lilikuwa halali kiroho kwa wao.Si unajenga tu bali kiwango cha kujenga ambacho Mungu anataka.Unajenga kwa ubora upi?.unajenga na kukaa nadani yake ni lazima ujenge na kutumia
4.OMBA MUNGU AKUPE KUTAMBUA MASHARTI YA KIROHO YALIYOP KWENYE ARDHI INAYOJENGWA JUU YAKE AU UNAYOKUSUDIA KUJENGA.kumb 8:7,11-12.
Katika sheria za umiliki kuna umiliki wa kiroho kwanza kabla ya umiliki wa kimwili.Sheria za umilikiwa kiroho zina nguvu kuliko za kimwili

Endelea kutufuatilia Gospel kitaa kwa Muendelezo wa Mafundisho

Share on Google Plus

About John Maulid

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.