UKWELI NI KWAMBA 'HATULEGEI' NJOO PTA SABASABA HAKUNA KIINGILIOHatimaye baada ya kusubiri kwa muda mrefu,  kazi njema kabisa iliyoandaliwa na kwaya mahiri katika medani ya muziki wa injili nchini Dar es salaam Gospel Choir (D.G.C) kutoka kanisa la Pentecostal Kurasini inayofahamika kwa jina la 'Hatulegei' inatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi huu.

Uzinduzi wa DVD hiyo ya 3 kutoka kwao DGC unatarajiwa kufanyika katika ukumbi mkubwa wa PTA uliopo katika viwanja vya maonyesho vya mwalimu JK Nyerere almaarufu kama Sabasaba jijini Dar es salaam tarehe 20 Novemba 2016 kuanzia majira ya saa 8 kamili mchana. Kati ya vikundi na waimbaji ambao watawasindikiza DGC ni pamoja na Uinjilisti Mtoni almaarufu kama LULU, Efatha Uhuru Moravian, The Reapers kutoka KLPT Kimara, Mwanamama Upendo Nkone, Kinondoni Revival Choir na waimbaji wengine wengi

Kwa mujibu wa DGC hakutakuwa na kiingilio  'HAKUNA KIINGILIO' siku hiyo, ili kuwapa nafasi wapenzi wa muziki wa injili kufika na kuweza kumtukuza na kumwabudu Mungu pamoja nao siku hiyo. DGC ni moja kati ya kwaya nchini ambazo uimbaji wao umetokea kuwabariki wengi tokea album yao ya kwanza 'Hakuna Jina Jingine' mpaka ya sasa. Kumbuka ni kwaya ambayo nyimbo zake za album ya kwanza zilipigwa na kuonyeshwa sana enzi hizo kupitia runinga ya EATV kila asubuhi. USIKOSE ni BURE Hebu onja wimbo uliobeba album 'HATULEGEI'


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.