WAIMBAJI WATATU KWETU PAZURI YA RWANDA WAPOTEZA BABA YAO HAPO JANA

Milly na Kaka yake Jimmy siku wazazi wao walipotimiza miaka kadhaa ya ndoa yao
Waimbaji watatu ambao ni ndugu wa kundi la Ambassadors of Christ ya Rwanda almaarufu kama 'Kwetu Pazuri, Jimmy, Betty pamoja na Milly wamefiwa na baba yao mzazi mzee Sam hapo jana jioni huku chanzo cha kifo chake kikiwa bado hakijajulikana.

Mzee Sam na mkewe enzi za uhai wake
Waimbaji Jimmy na Milly wamekuwa waimbishaji wa kwaya hiyo kwa muda mrefu toka wote watatu wajiunge kwaya hiyo mwishoni mwa miaka ya 90's. Mzee Sam ambaye pia alijaliwa kipaji cha ufundishaji wa muziki wa kwaya, amefanyika baraka katika kwaya mbalimbali nchini Rwanda pamoja na Uganda.

Kifo hicho ambacho kinaelezwa kuwa cha ghafla kimewaachia majonzi watoto hao kutokana na kutopata nafasi ya kuagana au kuwa pembeni ya baba yao wakati anaaga dunia. Kwasasa kwaya ya Ambassadors wapo kwenye matayarisho ya maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanza kwa huduma yao, maadhimisho ambayo yanatarajiwa kufanyika mwezi ujao nchini Rwanda huku wafiwa hao wakiwa miongoni mwa waimbaji muhimu katika kwaya hiyo. 

Ni miaka ya karibuni ambapo marehemu na mkewe mpenzi waliadhimisha miaka kadhaa ya ndoa yao, sherehe ambayo ilihudhuriwa na waimbaji wa Ambassadors of Christ, sambamba na watoto wa mzee huyo kwa pamoja wakiimba kwenye sherehe hiyo. Kama picha zote zilizotumika katika habari hii zikionyesha hali ilivyokuwa siku hiyo. 
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.

Waimbaji wa Ambassadors wakiimba siku hiyo


'Mtegemee Yesu'

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.